Thursday, September 19, 2019

“THE REVIEW OF THE NATIONAL INVESTMENT PROMOTION POLICY OF 1996” NATION-WIDE CALL FOR INPUTS

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 

PRIME MINISTER’S OFFICE

(POLICY, COORDINATION AND INVESTMENT) 


 “THE REVIEW OF THE NATIONAL INVESTMENT PROMOTION POLICY OF 1996” NATION-WIDE CALL FOR INPUTS 


The Government of the United Republic of Tanzania through the Prime Minister’s Office (Policy, Coordination and Investment) is undertaking the review of the National Investment Promotion Policy(NIPP) of 1996. This policy was formulated as part of the Government efforts in addressing the challenges facing the country in meeting its socio-economic aspirations given the resources and other intangible advantages that it enjoys. In addition, the review has been necessitated by various business and investment changes in the global, regional and national spheres since its inception in 1996. Moreover, the review will among others, form the basis for the formulation of the new National Investment Policy and its Implementation Strategy so as to align with and accelerate the realization of the aspiration of attaining the mid-income country as per Tanzania Development Vision 2025. Either, the process will sustain the country in optimizing the opportunities arising from the attainment of the middle income economy status.
Additionally, the Policy review process is embracing the principles of transparency, inclusiveness and consultation with all nationwide stakeholders. In that regard, the Government is hereby inviting the general public to submit their views, opinions and recommendations to foster the review process. The inputs provided will be treated with complete confidentiality and confined to this process only.
Inputs are invited, but not limited to the core areas identified here under: 

1.     Effective utilisation of national endowment
2.     Mobilization of domestic and international financing for investments 
3.     Provision of enabling physical infrastructure (Water, Electricity, Energy, Roadway, etc)
4.     Improvement of export competitiveness 
5.     Institutional framework to support investment development
6.     Land acquisition and ownership for investment
7.     Regulatory Framework including licensing, permits and approval processes for investment 
8.     Human capital development 
9.     Technological advancement and adoption 
10.  Investment incentives 
11.  Legal and Institutional Framework for investment
12.  Bilateral and Multilateral Investment Agreements and Treaties  
13.  Investment Disputes Settlements 


Kindly submit your inputs to Email: investmentpolicy@pmo.go.tzor Postal Address: Permanent Secretary, Prime Minister’s Office, (Policy, Coordination and Investment), P.O BOX 980, Government City, MtumbaDODOMA not later than 20thSeptember, 2019.

ISSUED BY THE GOVERNMENT COMMUNICATION UNIT 
PRIME MINISTER’S OFFICE, DODOMA-2NDSEPTEMBER,2019

Wednesday, September 18, 2019

PROF. KABUDI AMUAGA BALOZI WA RWANDA HAPA NCHINI MHE. KAYIHURA.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika katika Wazara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Wilbroad Kayombo akizungumza wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kwa jailli ya kumuaga Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura,ambaye amemaliza muda wake wa utumishi Nchini Tanzania. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kumuaga Balozi Kayihura ambaye amemaliza muda wake . Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza jambo wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa jailli ya kumuaga Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura ambaye amemaliza muda wake wa utumishi hapa nchini baada ya kuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura pamoja na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na wale wa Ubalozi wa Rwanda katika chakula cha pamoja kilichoandaliwa na Waziri,Prof. palamagam,ba John Kabudi kwa jailli ya kumuaga Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Kayihura ambaye amemaliza muda wake wa Utumishi. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kinyago cha umoja Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura ambaye amemaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura mara baada ya kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiagana na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene Kayihura mara baada ya kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi hapa Nchini. Balozi Kayihura amekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

Monday, September 16, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA NA MKURUGENZI WA AFRIKA NA UMOJA WA ULAYA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika,Wizara ya mambo ya Nje,Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania Mhe. Raimundo Robredo Rubio. Mazungumzo hayo yamelenga masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar Es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na mgeni wake ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Afrika,Wizara ya mambo ya Nje,Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania Mhe. Raimundo Robredo Rubio ( hayupo pichani) Mazungumzo yaliyolenga masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano  yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar Es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Afrika,Wizara ya mambo ya Nje,Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania Mhe. Raimundo Robredo Rubio akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo rasmi baina yao yaliyolenga kuimarisha mahusiano. Mazungumzo hayo  yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar Es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika,Wizara ya mambo ya Nje,Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania Mhe. Raimundo Robredo Rubio. kushoto ni Balozi wa Uhispania hapa Nchini Balozi Fransisca Maria Pedros Carretero panoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mkuu wa Afrika,Wizara ya mambo ya Nje,Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania Mhe. Raimundo Robredo Rubio pamoja na Balozi wa Uhispania hapa Nchini Balozi Fransisca Maria Pedros Carretero wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (Hayupo Pichani)
   






                 Umoja wa Ulaya watenga Euro bilioni 44 kusaidia nchi 10 za Afrika
Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania kupitia Mpango wa Tatu kwa Afrika "Third African Plan" umeahidi kusaidia nchi kumi za Afrika katika sekta za Maji, Afya, Utalii na Michezo.
Mkurugenzi Mkuu wa Afrika katika Wizara ya mambo ya Nje Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme Hispania, Bw. Raimundo Robredo Rubio amesema lengo la mkakati huo ni kusaidi nchi za Afrika, Tanzania ikiwa moja wapo ya nchi 10 zitakazo nufaika na mkakati huo. 
Aidha, Bw. Rubio ameongeza kuwa mkakati huo umelenga kutumia kiasi cha Euro bilioni 44 katika shughuli mbalimbali ikiwemo miradi ya Maji, ujenzi wa vituo vya Afya, uwekezaji katika sekta ya utalii na michezo.
"Kwa Tanzania miradi itakayo tekelezwa ni pamoja na mradi wa maji katika Halmashauri ya Mbozi, vijiji 12 kutoka kata ya Malangali Iringa na vituo mbalimbali vya Afya pamoja na michezo" Amesema Bw. Rubio
Bw. Rubio ameongeza kuwa Umoja wa Ulaya umelenga kutumia 'Mkakati wa Tatu kwa Afrika' ili kuimarisha ushirikiano katika nchi hizo ambapo pamoja na mambo mengine zitapata fursa ya kunufaika na miradi tajwa pamoja na uwekezaji kwa pamoja. 
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema hivi karibuni nchi ya Hispania imeona Afrika kama Bara lenye fursa ambapo moja kati ya nchi hizo ni Tanzania.
"Umoja wa Ulaya umeweka mkazo katika miradi ya maji, ujenzi wa vuto vya afya na hospitali na pia kuwekeza katika sekta ya utalii…Hispania ni moja ya nchi iliyopiga hatua kubwa sana katika sekta ya utalii barani Ulaya" Alisema Prof. Kabudi
Prof. Kabudi ameongeza kuwa Tanzania itashirikiana na Hispiania kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa ambapo kwa namna moja au nyingine nchi yetu itaendelea kuimarisha sekta hii muhimu. "Maeneo mengine ni sekta ya Michezo ambapo tunaamini pia kuimarisha sekta ya michezo, na kupata watawala wa michezo na waongozaji wa michezo hapa nchini watakuza kiwango cha mpira wetu," Amesema Prof. Kabudi
Kwa mujibu wa Bw. Rubio, nchi kumi za Afrika ambazo zinategemea kunufaika na fursa hiyo ni pamoja na Afrika Kusini, Nigeria, Ethiopia, Senegal, Ghana, Ivory Coast, Tanzania, Kenya, Angola and Msumbiji. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar Es Salaam,Tanzania
16 Septemba 2019

Saturday, September 14, 2019

KONGAMANO LA MADHIMISHO YA SIKU YA MARA LAFANYIKA




Balozi Ramadhan Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mara yanayondelea mjini Mugumu, Wilayani Serengeti. Kongamano hili linalojumuisha wadau kutoka Tanzania na Kenya, linalenga kujadili mustakabali wa bonde la Mto Mara na nafasi yake katika shughuli za uhifadhi.

Akizungumza katika kongamano hilo Balozi Mwinyi amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Kenya katika shughuli zote zinazolenga kujenga ustawi wa uchumi na jamii, na kuendeleza uhusiano imara uliopo baina ya nchi hizi mbili bila kusahau suala la uhifadhi wa mazingira ya bonde la Mto Mara.

Aidha amewataka wadau kuwa huru kutoa mawazo yao yanaoyelenga kutatua changamoto za uhifadhi zinazolikabiri bonde hilo sambamba na kuboresha jitihada na mikakati inayotumika sasa.

Kongamano hili linatarajiwa kutoa maazimio ambayo yatatoa uelekeo mpya na kuongeza kasi ya utekelezaji wa shughuli na jitihada za uhifadhi wa Bonde la Mto Mara.

Tarehe 15 Septemba, 2019 inatarajiwa kuwa siku ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mara yanayoendelea kufanyika mjini Mugumu wilayani Serengeti.
Meza kuu ikifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea wakati wa kongomano la Siku ya Mara lililofanyika katika ukumbi wa Kisarare mjini Mugumu, Serengeti


Balozi Ramadhan Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,akifuatilia jambo wakati kongamano likiendelea

Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, ambaye pia alikuwa mgeni wa heshima katika kongamano hilo akizungumza na hadhira iliyojitokeza (hawapo pichani) kujadili changamoto za uhifadhi wa Bonde la Mto Mara

SIKU YA PILI YA MAATHIMISHO YA SIKU YA MARA




Friday, September 13, 2019

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA WASHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI JIJINI CHENNAI

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akihutubia wakati wa Kongamano la kuvutia Biashara, Uwekezaji na Utalii lililofanyika katika hoteli ya Westin Jijini Chennai katika Jimbo la Tamil Nadu hivi karibuni. Kongamano hilo limeandaliwa na Shirikisho la Viwanda nchini India [Confederation of Indian Industry (CII) ambapo jumla ya wafanyabiasha 110 walihudhuria.
Kongamano likiendelea
Mhe. Balozi Luvanda (wa pili kulia) akiwa na Viongozi walioshriki Kongamano la kuvutia biashara, uwekezaji na utalii lililofanyika jijini Chennai nchini India
Meza kuu

========================================================================

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda amewakaribisha wafanyabiashara ba wawekezaji kutoka India kuja kuwekeza nchini kwani Tanzania imefanya mabadiliko makubwa katika sera zake za  kukuza biashara na kuvutia wawekezaji kutoka nje ikiwemo kuanzishwa kwa Wizara mahsusi inayosimamia masuala ya Uwekezaji.

Mhe. Balozi Luvanda ametoa rai hiyo wakati akihutubia Kongamano la kuvutia Biashara, Uwekezaji na Utalii lililofanyika katika hoteli ya Westin Jijini Chennai katika Jimbo la Tamil Nadu tarehe hivi karibuni. Kongamano hilo liliandaliwa na Shirikisho la Viwanda nchini India [Confederation of Indian Industry [CII] ambapo jumla ya wafanyabiasha 110 walihudhuria.

Mhe. Balozi Luvanda alieleza kuwa, kwa kiasi kikubwa mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini Tanzania yameboreshwa ikiwa ni pamoja na Serikali kufanyia kazi changamoto mbalimbali zilizokuwepo kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi. Jitihada hizo zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli za kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025.

Mhe. Balozi Luvanda alitumia fursa hiyo kuwaomba wafanyabiashara hao kuongeza ushirikiano na Tanzania katika  sekta ya biashara na utalii, hasa ikizingatiwa kuwa zaidi ya watalii milioni 20 wanaotembelea nchi mbalimbali duniani kwa mwaka wanatokea India, ikilinganishwa na watalii milioni 1.5 wanaoingia nchini Tanzania kwa mwaka.  
Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kutumia fursa ya kuanza safari za moja kwa moja za ndege za Shirika la Ndege la “Air Tanzania” kutoka Dar es Salaam kwenda Mumbai kuongeza idadi ya  watalii  wa India kutembelea Tanzania na kwa wawekezaji wake kuja kuwekeza katika hoteli na fukwe za Tanzania.



MAADHIMISHO YA SIKU YA MARA YAFUNGULIWA RASMI

     

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAADHIMISHO YA SIKU  YA MARA YAFUNGULIWA RASMI

Maadhimisho ya Siku ya Mara maarufu "Mara Day" yamefunguliwa rasmi tarehe 12 Septemba, 2019 na Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, katika uwanja wa Sokoine uliopo Mugumu, wilayani Serengeti. 

Maadhimisho haya yanayo adhimishwa kwa mzunguko kati ya nchi mbili za Tanzania na Kenya hufanyika kila mwaka, ambapo mwaka huu yanafanyika Tanzania katika Mji wa Mugumu wilayani Serengeti kuanzia tarehe 12 hadi 15 Septemba, 2019 yakiongozwa na kauli mbiu "Mimi ni Mto Mara, Nitunze Nikutunze".

 Madhimisho ya Siku ya Mara yanayolenga kuhimiza na kuhamasisha wananchi wanaozunguka bonde la mto Mara kuhifadhi mazingira ya mto, ili kulinda ikolojia ya bonde hilo ambalo ni muhimu kwa utastawi wa mazingira na uchumi wa jamii ya Tanzania na Kenya. Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa maadhimisho Mhe. Malima ambaye pia ni mgeni wa heshima katika sherehe hizo amesema, "ni jukumu la jamii na kizazi cha sasa kuhakikisha kuwa mazingira ya bonde la mto Mara yanaendelea kubaki salama na kustawi kwa mafuaa ya kizazi kilichopo na kijacho". 

Aidha, amewahamasisha  wananchi wa Mkoa wa Mara kuchangamkia fursa zinazotoka na maadhimisho hayo ikiwemo uuzaji wa bidhaa mbalimbali kwenye maonesho yanayoendelea  katika kipindi cha maadhimisho.

Maadhimisho ya Siku ya Mara yanafanyika ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afrika Mashariki la Bonde la Ziwa Victoria, uliofanyika terehe 4 Mei, 2012 jijini Kigali, Rwanda. Kilele cha maadhimisho haya hufanyika tarehe 15 Septemba kila mwaka ambayo pia inawiana na tukio la uhamaji wa wanyama pori kutoka Tanzania kwenda Kenya.

Bw. Eliabi Chodota Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, akizungumza na wanahabari amesisiza kuwa Serikali ya Tanzania na Kenya zimejidhatiti katika kuhifadhi bonde la mto Mara na kuwaasa wananchi wanaozunguka mazingira ya bonde hilo kuunga mkono jitihada za Serikali.
     
Maadhimisho haya yatakayofanyika kwa siku 4 yanahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo zoezi la upandaji miti ambapo, zaidi ya miti 500 itapandwa katika maeneo yanayozunguka bonde hilo. Vilevile yatahusisha uwekwaji wa alama za kuonesha mipaka ya ukomo wa shughuli za binadamu katika bonde hilo, mita kadhaa kutoka ukingo wa mto Mara.

Kwa mara ya kwanza maadhimisho haya yalifanyika tarehe 15 Septemba, 2012 mjini Mulot, Kenya yakiongozwa na kauli mbiu "Mara - Uhai wetu".


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam.
12 Septemba 2019
Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, akihutubia hadhira iliyojitokeza (hawapo pichani) kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Mara..
Moja ya banda linaloonesha na kuuza bidhaa za wajasiliamali katika maadhimisho ya siku ya Mara lililopo uwanja wa Sokoine - Mugumu, Serengeti.
Watendaji mbalimbali wa Serikali, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, na viongozi wa dini wakiwa tayari kumlaki mgeni wa heshima katika sherehe za ufunguzi Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara .
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya kuanza kwa sherehe za ufunguzi

Wednesday, September 11, 2019

BODI YA USHAURI YA UMOJA WA AFRIKA KUHUSU RUSHWA YAMTEMBELEA PROF. KABUDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Bodi ya ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu rushwa ikiwa ni ziara ya Bodi hiyo kutathmini utekelezaji wa mkataba wa Umoja wa Afrika dhidi ya rushwa.
Ujumbe wa bodi hiyo umeongozwa na Bw. Miarom Begoto.
Tanzania ni mwenyeji wa Bodi hiyo kupitia mkataba wa uenyeji kati take na Umoja wa Afrika ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni mratibu mkuu na msimamizi wa uytekelezaji wa shughuli za bodi.

Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu rushwa wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagmba John Kabudi (Mb) (Hayupo pichani)

Sehemu ya Ujumbe wa wa Bodi ya ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu rushwa wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagmba John Kabudi (Mb) (Hayupo pichani)

Kiongozi wa Ujumbe wa wa Bodi ya ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu rushwa Bw. Miarom Begoto akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagamba John Kabudi kijitabu chenye muongozo wa bodi hiyo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagamba John Kabudi na kiongozi wa Ujumbe wa Bodi ya ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu rushwa wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi hiyo alioambatana nao.

KATIBU MKUU EAC AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat Mfumukeko. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar Es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat mfumukeko akifuatilia mazungumzo baina yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) (hayupo pichani) Mazungumzo hayo yamefanyika wakati Katibu Mkuu huyo na ujumbe wake walipofika Jijini Dar es Salaam katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa nia ya kuzungumza masuala mbalimbali yanayoihusu Jumuiya hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) akifuatilia mazungumzo baina yake na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat mfumukeko. Mazungumzo hayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa nia ya kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu Jumuiya hiyo.

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat mfumukeko na Ujumbe wake wakifuatilia mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) (hayupo pichani) Mazungumzo hayo yamefanyika wakati Katibu Mkuu huyo na ujumbe wake walipofika Jijini Dar es Salaam katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa nia ya kuzungumza masuala mbalimbali yanayoihusu Jumuiya hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat Mfumukeko mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyolenga kujadili masuala mbalimbali kuhusu Juimuiya ya Afrika Mashariki.

Monday, September 9, 2019

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CUBA ZIARANI TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez. mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar Es Salaam.
Mazungumzo baina ya wawili hayo yamegusia mashirikiano katika nyanja za kidiplomasia,afya,elimu pamoja na viwanda.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimsikiliza mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez (hayupo pichani) Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar Es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani) katika Mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez wakiwa katika mazungumzo kuhusu mashirikiano baina ya nchi hizo mbili. wengine pichani ni Wakurugenzi na maafisa kutoka Tanzania na Cuba wakifuatilia mazungumzo haya yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.