Tuesday, February 13, 2024

DKT. MPANGO AONGOZA WAKAZI WA DAR eS SALAAM KUMUAGA HAYATI LOWASSA

 



 











Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ameongoza  waombelezaji  mbalimbali kutoka jijini Dar es Salam kuuaga mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa katika shughuli iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee tarehe 13 Februari, 2024.

Viongozi wengine waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu  wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman  Abdullah, Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk aliungana na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali, vyombo vya dola, viongozi wastaafu na wananchi katika shughuli hiyo ya kuaga mwili wa Hayati Lowassa. 

Hayati Edward Lowassa anatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Monduli, Arusha Februari 17, 2024 katika mazishi ya Kitaifa yanayotarajiwa kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayati Edward Lowassa alifariki dunia tarehe 10 Februari 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

 

 


Monday, February 12, 2024

MKUTANO WA 16 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA NISHATI WA AFRIKA MASHARIKI WAANZA JIJINI ARUSHA


Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Abdillah Mataka katika Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichangia hoja kwenye Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati wa EAC uliokuwa ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha.

Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umenza leo tarehe 12 Februari 2024 katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha. 

Mkutano huo wa siku tatu kuanzia February 12 hadi 14, 2024 utafanyika katika ngazi tatu; ngazi ya Wataalamu tarehe 12 Februari 2024, ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 13 Februari 2024 na kuhitimishwa katika ngazi ya Mawaziri tarehe 14 Februari 2024.

Mkutano huo unatarajiwa kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nishati katika Jumuiya. Vilevile kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua chagamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika na endelevu katika Jumuiya. 

Maeneo ya sekta ya nishati yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni; umeme, mafuta na nishati jadidifu. 

Awali akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa ngazi ya wataalamu Mwenyekiti wa Mkutano huo Bw. Petro Lyatuu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Nishati – Tanzania ameeleza kuwa licha ya mafanikio yaliyofikiwa katika sekta hiyo bado mchango na weledi wa wataalamu hao unahitajika ili kutatua changamoto zilizopo na hatimaye kufikia malengo yanayotarajiwa na Jumuiya. 

Bwana Lyatuu ametoa rai kwa watalamu hao kujikita katika kujadili na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu masuala muhimu yatakayojili katika mkutano huo kwa manufaa ya Jumuiya.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa ngazi ya wataalamu unaongozwa na Bw. Abdillah Mataka Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Mkutano huo unatarajiwa hutimishwa tarehe 14 Februari 2024 katika ngazi ya Mawaziri wanaosimamia sekta ya nishati umehudhiriwa na wajumbe kutoka Nchi zote saba (7) wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Nishati Bw. Petro Lyatuu akiongoza Mkutano wa 16 Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati uliokuwa ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mkutano wa 16 Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati uliokuwa ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mkutano wa 16 Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati uliokuwa ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha




 Mkutano wa 16 Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha

Saturday, February 10, 2024

WANANCHI TOENI MAONI KWA AJILI YA SERA YENYE TIJA, WAZIRI


Makongamano ya wadau yanayoendelea nchini kuhusu marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 yanalenga kukusanya maoni yatakayosaidia kutengeneza Sera ya Mambo ya Nje Bora itakayoongoza ushirikiano wenye tija baina ya Tanzania na nchi nyingine, mashirika ya kikanda na kimataifa.

Hayo yamesemwa leo tarehe 10 Februari 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu - Zamzibar, Mhe. Ali Suleiman Ameir wakati akisoma hotuba ya ufunguzi ya Kongamano la nne la wadau lililofanyika kisiwani Pemba.

Makongamano hayo yanayoratibiwa kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ofisi ya Rais-Zanzibar na Taasisi ya Uongozi yametajwa kuwa ni kielelezo cha utawala bora ambao unahimiza ushirikishwaji wa wananchi katika utengenezaji wa Sera za Taifa.

Akizungumza katika kongamano hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) amesisitiza umuhimu wa wananchi walioshiriki kongamano hilo kutoa maoni yao kwa uhuru bila woga. Alisema maoni yao yatasaidia kutengeneza Sera ya Mambo ya Nje madhubuti itakayoifanya Tanzania kutetea maslahi yake katika majukwaa ya Kimataifa na kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika dunia ya sasa.

Alisema mijadala yao ya kurekebisha Sera ya Mambo ya Nje itatoa mwelekeo wa kuboresha maeneo mapya yanayopendekezwa ambayo ni pamoja na masuala ya uchumi wa Buluu, diaspora, mabadiliko ya tabianchi, kubidhaisha Lugha ya Kiswahili na kulinda mila na desturi za Tanzania.

Balozi Mbarouk alimsifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji mzuri wa Sera ya Mambo ya Nje ambao umesaidia kuongezeka kwa ajira za Watanzania katika mashirika ya kikanda na Kimataifa, masoko ya bidhaa za Tanzania Nje ya nchi, misaada na mikopo ya Maendeleo, uenyeji wa taasisi za kimataifa nchini na ujenzi wa miradi ya Maendeleo katika sekta mbalimbali za miundombinu, nishati, kilimo, elimu na afya.

Kongamano hilo ambalo ni mwendelezo wa makongamano yaliyofanyika Arusha, Dar Es Salaam na Unguja limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kusini-Pemba, Mhe. Matar Zahor Masoud; Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Zanzibar, Bw. Salehe Juma Mussa, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shwaibu Mussa; baadhi ya Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi; wawakilishi wa vyama vya siasa; asasi za kiraia; jumuiya za kidini na wananchi kwa ujumla.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu-Zanzibar, Mhe.  Ali Suleiman Ameir akitoa hotuba ya ufunguzi ya Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Pemba tarehe 10 Februari 2024

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akizungumza na wadau walioshiriki katika kongamano la kutoa maoni kuhusu marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Pemba tarehe 10 Februari 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu - Zanzibar, Mhe. Ali Suleiman Ameir akisalimiana na na baadhi ya viongozi wa Serikali na wajumbe walioshiriki Kongamano la kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Pemba tarehe 10 Februari 2024

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Ikulu Zanzibar, Bw. Salehe Juma Mussa akitoa neno wakati wa Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Pemba tarehe 10 Februari 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu - Zanzibar, Mhe. Ali Suleiman Ameir (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) ambao walikuwa wenyeviti wenza katika Kongamano la kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Pemba tarehe 10 Februari 2024

Kongamano la kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Pemba tarehe 10 Februari 2024 likiendelea.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali na wajumbe walioshiriki Kongamano la kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Pemba tarehe 10 Februari 2024

Friday, February 9, 2024

RAIS WA POLAND ATEMBELEA HOSPITALI YA AGHAKHAN

 

Rais wa Jamhuri ya Poland Mheshimiwa Andrzej Duda akizungumza bada ya kutembelea mradi wa matibabu ya dharura unaoendeshwa katika hospitali ya Aghakhan jijini Dar es Salaam ili kujionea utekelezaji wa mradi huo.

Rais wa Jamhuri ya Poland Mheshimiwa Andrzej Duda (mwenye tai nyekundu) na Mke wake Bibi Agata Kornhouser-Duda (kushoto) walipotembelea mradi wa matibabu ya dharura unaoendeshwa katika hospitali ya Aghakhan jijini Dar es Salaam ili kujionea utekelezaji wa mradi huo.


Mke wa Rais wa Poland  Bibi Agata Kornhouser-Duda akizungumza kitu walipotembelea mradi wa matibabu ya dharura unaoendeshwa katika hospitali ya Aghakhan jijini Dar es Salaam ili kujionea utekelezaji wa mradi huo




 

 

Rais wa Jamhuri ya Poland Mheshimiwa Andrzej Duda na Mke wake Agata Kornhouser-Duda wametembelea mradi wa matibabu ya dharura unaoendeshwa katika hospitali ya Aghakhan jijini Dar es Salaam ili kujionea utekelezaji wa mradi huo.

Kupitia Mradi huo Serikali ya Poland imetoa msaada wa Dola za Marekani 1,136,703 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa mradi huo unaolenga kutoa msaada kwa sekta ya matibabu na kusaidia elimu ya wahudumu wa afya katika mkoa wa Dar es Salaam.

Poland pia inafadhili miradi kama hiyo katika Hospitali za Temeke, Mwananyamala, kituo cha Afya Chamazi na Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana ya mkoani Mwanza.

 

TANZANIA – POLAND KUENDELEA KUSHIRIKIANA KIUCHUMI

Rais wa Jamhuri ya Poland Mhe. Andrzej Duda akisalimia na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Poland Mhe. Andrzej Duda akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam huku mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan akimuangalia

Rais wa Jamhuri ya Poland Mhe. Andrzej Duda akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Poland Mhe. Andrzej Duda akizungumza na waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam

 Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Jamhuri ya Poland Mhe. Andrzej Duda wakizungumza na waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaamkuelezea waliyokubaliana kutekeleza baada ya mazungumzo yao



Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Poland zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika sekta za kimkakati ikiwemo elimu, kilimo, biashara na uwekezaji ili  kukuza uchumi kwa manufaa ya pande zote mbili.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Poland, Mhe. Andrzej Duda walipozungumza na waandishi wa habari Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano huo,  Mhe. Rais Samia ameeleza kuwa Tanzania na Poland zimekuwa na ushirikiano mzuri kwa zaidi ya miaka 60 huku wakishirikiana kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hususan katika sekta ya Afya.

“Poland inatusaidia katika sekta ya afya, kuna miradi mitano ambayo Poland inafadhili katika Hospitali za Agah Khan, Kituo cha afya cha Chanika, Hospitali ya Temeke, Mwananyamala na Hospitali ya wilaya ya Nyamagana,” alisema Mhe. Rais Samia

Amesema wamekubaliana na Poland kuendelea kushirikiana katika sekta za kimkakati za elimu, kilimo, nishati, madini, biashara, uwekezaji na utalii

 “Katika mazungumzo yetu tumeelekeza timu za pande zote mbili kukaa na kufanya majadiliano ya mara kwa mara ili kubaini maeneo mapya ya ushirikiano ambayo yatatusaidia kupiga hatua kwa haraka zaidi katika kukuza biashara na uwekezaji na utalii kwa manufaa ya watu wetu” Alisema Rais Samia.


Ameishukuru Poland kupitia Wakala wake wa Mikopo kwa kukubali kuipatia Tanzania mkopo utakawezesha ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR ambapo itahusisha ujenzi wa Lot 3 na Lot 4.

Hii ni hatua kubwa sana katika kutekeleza miradi ya kimkakati ambao pia utasaidia kukuza ujuzi wa wataalam wetu, tunawashukuru sana  kwa kukubali kutupatia mkopo huo,” alisema Mhe. Rais Samia.

Amesema wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania kutoka Poland pamoja na kuinua kiwango cha biashara na kuvutia wawaekezaji zaidi kutoka Poland.

Amesema wamekubaliana kuwa wataalam wao watazungumza na kukubaliana namna bora na kuanzisha usafiri wa moja kwa
moja kutoka Poland hadi Tanzania haÅŸa ikizingatiwa kuwa kuna idadi kubwa ya watalii kutoka Poland wanaokuja nchini.

“Kumekuwa na ongezeko la watalii ambapo kwa mwaka 2023 tulipokea watalii 41,000 na kwa mwezi mmoja tu uliopita tulipokea watalii 6,000 walioenda visiwani Zanzibar kutalii,” alisema.

Amesema amewakaribisha wawekezaji kutoka Poland waje Tanzania kwani fursa za uwekezaji ni nyingi.

Naye Rais Duda akizungumza katika mkutano huo ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na Poland kitendo ambacho kilianza tangu wakati wa vita ya pili ya ambapo Tanzania iliwapokea raia wa Poland waliokuja Tanzania kutafuta Hifadhi wakati huo

Amewashukuru wananchi wa Arusha kwa kuendelea kuishi na   wananchi wa Poland na kuyaenzi makaburi ya watu hao.

Kadhalika amesisitiza kuwa, atahakikisha utalii, uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Poland unaongezeka kwani anajua Tanzania ni kituo kinachovutia na anaamini kuwa kuongezeka huko kutasaidia kutengeneza ajira kwa vijana, kuongeza ufanisi kwa kuleta mifumo ya kisasa ya kuendesha benki.

Ameahidi kuwa atahakikisha kampuni ya Poland ambazo zipo vizuri katika teknolojia ya mawasiliano zinakuja kwa wingi kuwekeza nchini.

“ Kwa kuanzia tutaanza na kampuni inayotengeneza Taa za nishati mbadala tutaangalia jinsi kampuni hiyo inakuja Tanzania kuwekeza,” alisema Mhe. Rais Duda.

RAIS WA POLAND APOKELEWA RASMI IKULU

 

 

 

 

 

Rais wa Jamhuri ya Poland Mhe. Andrzej Duda akisalimiana na mwenyeji wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa rasmi 

 Mhe. Rais Duda alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake  Rais Samia Suluhu Hassan
 

Mheshimiwa Rais Andrzej Duda wa Poland akikagua gwaride la heshima katika hafla ya kumkaribisha Tanzania iliyofanywa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 9 Februari, 2024.

Mheshimiwa Rais Andrzej Duda wa Poland akikagua gwaride la heshima katika hafla ya kumkaribisha Tanzania iliyofanywa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 9 Februari, 2024.

Mheshimiwa Rais Andrzej Duda wa Poland akikagua gwaride la heshima katika hafla ya kumkaribisha Tanzania iliyofanywa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 9 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Poland Mhe. Andrzej Duda akipokea salamu za heshima na mwenyeji wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa rasmi 

 
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa serikali waliposhiriki mapokezi rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Poland Mhe. Andrzej Duda aalipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa rasmi 

Rais wa Jamhuri ya Poland, Mheshimiwa Andrzej Duda amepokelewa rasmi Ikulu, jijini Dar es Salaam na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Alipowasili Ikulu Mhe. Rais Duda alipigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride  lililoandaliwa maalum kwa heshima yake  kuungana na Mhe. Rais Samia katika mazungumzo ya  faragha
 

Mhe. Rais Duda yuko nchini kwa Ziara ya Kitaifa ya siku mbili na kuwa Rais wa kwanza wa Poland kufanya ziara ya Kitaifa Tanzania

 



DKT. SHELUKINDO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA KAMATI YA SIASA NA DIPLOMASIA YA SADC

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Kamati ya Siasa na Diplomasia (Inter-State Politics and Diplomacy Committee — ISPDC) ya SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 09 Februari, 2024.

Mkutano huo umeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Zambia, Bi. Etambuyu Gundersen ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.

Mkutano huo uliitishwa kujadili masuala ya kisiasa na diplomasia katika kanda. Aidha, Mkutano umetoa salamu za pole kwa Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Namibia kufuatia kifo cha Hayati Dkt. Hage Geingob, Rais wa Jamhuri ya Namibia na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kilichotokea hivi karibuni.






RAIS WA POLAND AWASILI TANZANIA KWA ZIARA YA KITAIFA

 











Rais wa Jamhuri ya Poland, Mheshimiwa Andrzej Duda amewasili nchini kwa Ziara ya Kitaifa ya siku mbili.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais Duda na mkewe Agata Kornhauser-Duda wamepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrick Soraga na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Ziara hii ni ya kwanza kwa Rais kutoka Poland kutembelea Tanzania tangu kuanza kwa ushirikiano wa uwili kati ya nchi hizi ikilenga kuimarisha ushirikiano katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta za kilimo, kodi, viwanda na biashara, utalii, elimu, usafiri, afya, tiba za mifugo, na maji.

Kwa kupitia ziara hii maeneo mapya ya ushirikiano yataibuliwa kati ya Tanzania na Poland kupitia sekta za ulinzi na usalama, nishati, madini, ulinzi wa mitandao, utamaduni na uchumi wa buluu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan atampokea rasmi Rais Duda Ikulu, Dar es salaam Februari 9, 2024 kwa mazungumzo na baadaye watazungumza na waandishi wa habari.

Akiwa nchini, Rais Duda anatarajiwa kutembelea mradi wa matibabu ya dharura katika Hospitali ya Aghakhan, Dar es Salaam kujionea utekelezaji wa mradi huo ambao Serikali ya Poland imetoa msaada wa Dola za Kimarekani milioni 1.136  kufadhili mradi huo wenye lengo la kutoa msaada kwa sekta ya matibabu na kusaidia elimu ya wahudumu wa afya katika mkoa wa Dar es Salaam.




Thursday, February 8, 2024

DKT. KIBESSE ATETA NA GAVANA WA KAUNTI YA KISUMU

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Bernard Kibesse amefanya ziara katika Kaunti ya Kisumu ambapo pamoja na mambo mengine, amekutana kwa mazungumzo na Gavana wa Kaunti ya Kisumu – Kenya, Mhe. Prof. Peter Nyon’go, tarehe 8 Februari 2024. 

 Balozi Kibese na Gavana Nyong’o wamekubaliana kuandaa mkutano wa ujirani mwema kati ya mikoa ya Tanzania na Kenya inayopakana kwenye eneo la Ziwa Victoria ili kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa kijamii, kibishara na kiusalama katika maeneo hayo ikiwemo mikoa ya Mwanza na Mara kwa upande wa Tanzania na Kisumu na Migori kwa upande wa Kenya

Vilevile wamekubaliana kufuatilia mpango wa kuwa na miundombinu ya barabara inayopita kwenye mwambao wa Ziwa Victoria upande wa Tanzania na Kenya.

Gavana wa Kaunti ya Kisumu – Kenya, Mhe. Prof. Peter Nyon’go akizungumza na  Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Bernard Kibesse (kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake katika Kaunti ya Kisumu




WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA KATIBU WA NEC SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA WA CCM

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Katibu wa NEC Siasa na uhusiano wa kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdallah Hamid katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Lengo la kikao cha viongozi hao ni kuangalia jinsi ambavyo Wizara inavyotekeleza Diplomasia ya Uchumi na uhusiano wa Kimataifa kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).