Tuesday, May 10, 2016

Mabalozi kutoka nchi za Ghuba watembelea Wizara ya Mambo ya Nje

 Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima  akizungumza na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kiongozi wa kundi la Mabalozi kutoka nchi za Ghuba nchini Tanzania, Mhe. Abdullah Ibrahim Ghanim Al Suwaidi, Mabalozi hao ambao hawapo pichani walimtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa madhumuni ya kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za kiarabu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa katika sekta za uchumi.
Kutoka kushoto ni Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Wajih Alotaabi, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Ibrahim Al- Najem, Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Soud Ali Mohamed Al Ruqaishi na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe. Abdallah Jassim Al- Madady. 
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea, kutoka kushoto ni Bw.Hangi Mgaka na Bw. Tahir Khamis
Waheshimiwa Mabalozi na maafisa wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.