TAARIFA
KWA UMMA
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kutoa utaratibu wa matumizi ya Bendera
na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
kama ilivyotangazwa hivi karibuni.
Utaratibu huo ni kwamba Bendera ya Taifa itaanza kupeperushwa
ikifuatiwa na Bendera ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki, vivyo hivyo Wimbo wa Taifa utaanza kupigwa ukifuatiwa na Wimbo
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilitatangaza kuhusu
matumizi ya Bendera na Wimbo wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki katika Wizara, Idara, Mashirika na Taasisi mbalimbali za
Serikali pamoja na Taasisi Binafsi.
Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
unapatikana katika tovuti ya Wizara ambayo ni www.foreign.go.tz.
Aidha, kwa mujibu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki vipimo maalum vya
kutengeneza Bendera hiyo ni kama vinavyoonekana hapa chini.
Imetolewa na,
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 23 Mei, 2016.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.