Waziri wa Mambo ya nje Ushirikano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (aliye shikilia funguo za gari), akipokea Ufunguo wa Magari ya Wagonjwa kutoka kwa Balozi wa Korea Kusini nchini, Mhe. Song Geum Young yaliyotolewa Serikali ya nchi yake. Waziri Mahiga alitumia nafasi hiyo Kuishukuru na kuipongeza Serikali ya Korea Kusini kwa msaada huo ambo utatumika kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza. Tanzania na Korea Kusini zina mahusiano mazuri, ambapo Korea Kusini inaendelea kuisaidia Tanzania kwenye sekta mbalimbali zikiwemo afya,miundombinu, elimu na uchumi. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.