Tuesday, May 10, 2016

Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za Tanzania na Zambia wakutana kwa mazungumzo

  
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Aziz Mlima akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Zambia, Bw. Chalwe Lombe ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana. Wawili hao walizungumzia umuhimu wa kudumisha na kuimarisha ushirikiano ambao ulianzishwa tokea enzi za waasisi wa mataifa haya mawili. Walisema Waasisi wa Mataifa haya waliweka misingi bora ya ushirikiano ikiwemo ujenzi wa reli ya TAZARA inayounganisha nchi hizi mbili ambayo ilifadhiliwa na serikali ya watu wa China na kuwa msaada mkubwa katika kurahisisha shughuli za kibiashara.
Mhe. Lombe akielezea fursa za kiuchumi zilizopo nchini Zambia kama vile mazao ya kilimo na madini na kuelezea matumaini yake kuwa mpango wa kufanya maboresho na upanuzi wa Reli ya TAZARA utasaidia kukuza uchumi kati ya Tanzania na Zambia kwakuwa wananchi wataweza kufanya biashara pasipo na usumbufu.
Wanaofuatilia mazungumzo kutoka kushoto ni Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Judith Kapijimanga na wa pili kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Halima Abdallah.
Makatibu Wakuu wakiagana mara baada ya mazungumzo

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.