Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano ambao Bi. Kasiga aliwaelezea mafanikio ya ziara iliyofanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Aziz Mlima nchini China ambapo pamoja na kufadhili shughuli mbalimbali za kiuchumi, nchi hiyo pia imekubali kutoa ufadhili wa nafasi kumi za masomo ya kidiplomasia ambapo itatoa nafasi tano za mafunzo ya muda mrefu na tano za muda mfupi kwa kila mwaka
==================================================================
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Ziara
ya Kikazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
nchini China
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz
Mlima alifanya ziara ya kikazi nchini China kuanzia tarehe 15 – 19 Mei 2016
kufuatia mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo. Lengo la ziara hiyo
lilikuwa ni kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na China katika nyanja za
siasa, uchumi na utamaduni.
Akiwa
nchini China, Dkt. Mlima pamoja na mambo mengine alipata fursa ya kufanya
mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Makampuni makubwa ya China
ambayo baadhi yao yameshawekeza nchini na mengine yameonesha dhamira ya
kuwekeza.
Wakati
wa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Zhang Ming,
masuala mbalimbali yalijitokeza ikiwa ni pamoja na China kusisitiza dhamira
yake ya dhati ya kukuza ushirikiano na Tanzania katika nyanja ya uchumi kupitia
uwekezaji kwenye sekta ya viwanda, nishati na miundombinu. China imeweka
kipaumbele cha juu katika miradi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na eneo la
viwanda pamoja na maboresho ya Reli ya TAZARA na ipo tayari kuanza upembuzi
yakinifu wa Reli ya Kati.
Kwa
upande wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Kampuni ya China ya Merchant Holding
International (CMHI) ambayo imeingia ubia na Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Oman
kujenga bandari hiyo, wapo katika hatua nzuri ya kukamilisha mazungumzo ya ubia
wao ili waanze awamu ya kwanza ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ndani ya mwaka
huu wa 2016.
Kwa
suala la ujenzi wa eneo la viwanda, Serikali ya China imebainisha kuwa ikwishatenga
fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu wezeshi (barabara, nishati ya umeme,
maji, TEHAMA).
Kuhusu
Reli ya TAZARA, China imeahidi kuwa itaendelea kuipa kipaumbele cha juu reli
hiyo kwa sababu inabeba historia ya mahusiano yake na Afrika. China imeridhishwa
na mazungumzo ya wataalamu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni na
kuahidi kufanyia kazi yaliyokubalika ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kupitia
Itifaki ya 16 kwa ajili ya maboresho makubwa ya miundombinu ya TAZARA pamoja na
kushiriki kikamilifu kwenye mikutano itakayofuata kuangalia namna bora ya
kuendesha reli hiyo kwa ushirikiano na Tanzania na Zambia.
Mkutano na Mamlaka ya Tumbaku
Katibu
Mkuu alikutana na Kamishna wa State
Tobacco Monopology, Bw. Lin Chengxing ambapo pamoja na mambo mengine
walizungumzia utekelezaji wa Mkataba wa Kuruhusu Tumbaku ya Tanzania kuingia
soko la China uliosainiwa mwaka 2013 wakati Rais wa nchi hiyo, Mhe. Xi Jinping
alipofanya ziara nchini. Bw. Lin alijulisha kwamba makampuni mawili ya
China-Hunan Industries na Shandong Industries yamepewa jukumu la kuinunua
tumbaku ya Tanzania kwa ajili ya kufanya majaribio.
Hadi hivi sasa wameshanunua
tani 1500 ambazo zinahifadhiwa kwa kati ya miezi 24 hadi 30 (fermentation)
kabla ya kutumika kuzalisha sigara. Matarajio yao ni kwamba sigara
zitakazozalishwa na tumbaku ya Tanzania itaingia soko la China mwaka ujao.
Endapo soko la China litapendelea sigara hizo, mahitaji ya tumbaku ya Tanzania
katika soko la China yataongezeka kwa kiasi kikubwa.
Mkutano na Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje
Dkt.
Mlima alikutana na Rais wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China, Prof. Qin
Yaqing ambapo walijadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya chuo hicho
na Chuo cha Diplomasia cha hapa nchini. Katika majadiliano hayo, walikubaliana kushirikiana katika tafiti na
utoaji wa mihadhara. Aidha, Chuo hicho
kimeahidi kutoa nafasi za masomo tano za muda mfupi na tano za muda mrefu kila
mwaka kwa Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia na watumishi wa Wizara ya Mambo ya
Nje. Chuo hicho kilianzishwa mahsusi kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa wa
Wizara ya Mambo ya Nje ya China na baadaye kilianzisha programu mbalimbali na
kuchukua wanafunzi kutoka nje ya nchi.
Imetolewa na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar
es Salaam,
26 Mei 2016.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.