Saturday, July 20, 2013

Miili ya Askari waliofariki mjini Darfur yawasili nchini


Sehemu ya Masanduku yenye miili ya askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia hivi karibuni mjini Darfur nchini Sudan wakati wakilinda amani, yawasili nchini leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.  

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wanananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia mjini Darfur wakati wakilinda amani.  

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wanananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipakia moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia mjini Darfur wakati wakilinda amani.  

Askari hao waliuwawa kwa shambulio la kushtukiza na kundi la waasi wakati wakiwa kwenye kazi yao ya kulinda amani nchini Sudan.  

Jeshi la JWTZ lilioa taarifa likisema kuwa tukio hilo ni pigo kubwa kwa nchi yetu ya Tanzania ikiwa ni la kwanza kutokea tangu Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007.


Picha na maelezo kwa hisani ya www.issamichuzi.blogspot.com




Friday, July 19, 2013

Mhe. Membe akutana na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu wa China


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Liu Jiayi alipofika Wizarani na Ujumbe wake kwa mazungumzo kuhusu Serikali hizi mbili kushirikiana kwa kubadilishana uzoefu katika masuala ya ukaguzi wa hesabu za serikali.
Bw. Liu Jiayi (wa kwanza kulia) na ujumbe wake akiwemo Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lv Youqing (wa tatu kutoka kulia) wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo nae.
Bw. Liu Jiayi akimweleza jambo Mhe. Membe aliyekuwa akisikiliza kwa makini.

Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Ludovick Utoh na ujumbe wake wakimsikiliza Bw. Lui Jiayi (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na Mhe. Membe.

Mhe. Membe na wajumbe kutoka Tanzania na China kwa pamoja wakimsikiliza Bw. Liu Jiayi.

Mhe. Membe na Bw. Utoh wakimsikiliza Bw. Liu Jiayi alipokuwa akifafanua jambo katika moja ya taarifa za ukaguzi za nchini kwake alizomkabidhi Mhe. Membe.

Bw. Adam Isara, Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Bw. Liu Jiayi.
Mhe. Membe katika picha ya pamoja na Bw. Liu Jiayi na Mhe. Balozi Lv Youqing.

Mhe. Membe akiagana na Bw. Liu Jiayi.





Mhe. Balozi Mulamula awasilisha Hati za Utambulisho


Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Barack Obama, Rais wa Marekani mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho katika Ikulu ya nchi hiyo (The White House) mjini Washington, DC. 

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akijiandaa kwenda kuwasilisha hati za utambulisho kwenye Ikulu ya Marekani (The White House) iliyopo mjini Washington, DC. 

Mhe. Balozi Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na familia yake wakiwemo Mumewe Bw. George Mulamula na watoto wake Bi. Tanya na Bw. Alvin.

Mhe. Balozi Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na familia yake wakiwemo Mumewe Bw. George Mulamula na watoto wake Bi. Tanya na Bw. Alvin.



Thursday, July 18, 2013

Balozi Kairuki akutana na Wakurugenzi wa JETRO


Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mberwa Kairuki (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Biashara ya Nje ya Japan (Japan External Trade Organization-JETRO) ofisi ya Nairobi, Kenya, Bw. Hiroshi Komatsuzaki (kushoto). Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa JETRO ofisi ya Johannesburg, Afrika Kusini, Bw. Kimihiko Inaba. Wakurugenzi hao walionana na Balozi Kairuki jijini Dar es Salaam kuzungumzia ziara ya Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan  itakayofanyika nchini mwezi Agosti, 2013.
 
picha ya pamoja ya ujumbe wa Tanzania na JETRO wakiwa katika mazungumzo


Maafisa wa Mambo ya Nje katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Khatibu Makenga na Bibi Redemptor Tibaigana wakinuu masuala muhimu ya mazungumzo.

Ujumbe wa Japan katika mazungumzo hayo, kutoka kulia ni Bw. Kimihiko, Bw. Hiroshi na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya kati na Afrika wa JETRO, Bw. Shintaro Matoba.


Wednesday, July 17, 2013

Balozi Kairuki akutana na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika wa China


Mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (kulia)akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Bw. Lu Shaye. Bw. Lu ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya China ya  kufuatilia masuala yaliyokubaliwa wakati wa Mkutano wa FOCAC  alikutana na Balozi Kairuki kujadili namna Tanzania ilivyojipanga kuchangamkia ahadi zilizotolewa na China kwa nchi za Afrika wakati wa Mkutano wa FOCAC. 


Balozi Kairuki (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo huku Bw. Lu akisikiliza kwa makini.


Picha ya pamoja kati ya  ujumbe wa Bw. Lu na ujumbe wa Balozi Kairuki wakiwa katika mazungumzo.
 Picha na Reginard P. Kisaka

Tuesday, July 16, 2013

TANZIA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi wake Bw. Dismas Mathias Kajogoo, Afisa Mawasiliano Mkuu kilichotokea Moscow, Urusi

Taarifa ya kusafirisha mwili wa Marehemu kuja Tanzania kwa ajili ya mazishi itatolewa baadaye.


BWANA AMETOA NA BWANA AMETWA, JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE. AMEN.

Monday, July 15, 2013

Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wahudhuria Mkutano wa Afrika kujadili magonjwa mbalimbali


Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mfalme Mswati wa Swaziland III, wakati wa Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) nchini Nigeria.  Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan tarehe 15 Julai 2013 mjini Abuja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akishiriki katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja + 12) nchini Nigeria.  Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mhe. Mahadhi Juma Maalim (MB) (nyuma kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 


Picha na OMR, kwa hisani ya michuzi blog 


TAMKO LA RAIS KIKWETE KUHUSU VIFO VYA WANAJESHI 7 SUDANI



Tamko la Rais na Amiri Jeshi Mkuu kuhusu tukio la Darfur

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa sana na tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa vijana saba hodari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania waliokuwa wanalinda amani katika eneo la Darfur, Sudan.

Kwa hakika, Rais amesikitishwa sana na kitendo hicho ambako wanajeshi wengine 14 wa Tanzania wamejeruhiwa na waasi wa Sudan na ametuma salamu za rambirambi za moyoni mwake kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kwa familia za wafiwa wote.

Aidha, Rais Kikwete anaungana na Watanzania wote na hasa maofisa na wapiganaji wa JWTZ na familia za wafiwa kuomboleza vifo vya vijana hao hodari wa Tanzania. Rais pia anaungana na Watanzania wote kuwaombea wale walioumia katika tukio hilo waweze kupona haraka na kuendelea na majukumu yao ya 
ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.

Katika salamu zake za rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Adolf Mwamunynge na familia za wafiwa, Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu amesema:
“Sina maneno ya kutosha ya kuelezea mshtuko, huzuni na masikitiko yangu makubwa kufuatia vifo vya vijana wetu hao ambao wamepoteza maisha yao katika shughuli muhimu sana ya utekelezaji wa majukumu ya Umoja wa Mataifa ya kulinda na kuleta amani katika eneo la dunia ambako maelfu kwa maelfu ya watu wamepoteza maisha yao kwa kushambuliwa na waassi.”

Rais Kikwete ameongeza kumwambia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na familia za wafiwa ”Napenda kwa niaba ya Watanzania wenzangu niwahakikishieni kwamba hakuna shaka kuwa vijana wetu hao tokea walipokwenda  Darfur Februari mwaka huu, na kwa hakika tokea Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi katika eneo hilo mwaka 2007, wamefanya kazi nzuri sana, kazi iliyoongozwa na weledi wa hali ya juu na kazi ambayo imeiletea nchi yetu heshima kubwa. Tutaendelea kuwaenzi kwa kujivunia kazi yao.”

Amesisitiza Mheshimiwa Rais Kikwete: “Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza vijana wetu hawa. Kupitia kwao, natuma salamu za rambirambi kwa maofisa wakuu na maofisa wadogo pamoja na wapigaji wote wa Jeshi letu kwa kupotelewa na wenzao. “

“Aidha, kupitia kwako, natuma salamu zangu kwa wanafamilia za waliopotelewa na wapenzi wao na ndugu zao katika tukio hilo. Wajulishe kuwa naungana nao katika kuomboleza. 

Wajue kuwa uchungu wao ni uchungu wangu pia na wa Watanzania wote na kuwa kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu. Vile vile kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu azilaze peponi roho za marehemu. Amina”.

Kwa walioumia, Rais Kikwete amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Naungana pia na Watanzania wenzangu katika kuwapa pole nyingi walioumia katika tukio hilo tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na kuendelea na shughuli zao za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.”

Vijana hao waliopoteza maisha yao na walioumia, walikuwa sehemu ya askari 37 na ofisa mmoja ambao walikuwa wanasindikiza msafara wa waangalizi wa kijeshi katika Darfur kutoka eneo la Khorabeche kwenda Nyara waliposhambuliwa na waasi kiasi cha kilomita 20 kutoka Khorabeche saa tatu asubuhi jana, Jumamosi, Julai 13, 2013.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

14 Julai, 2013


UN Chief condemns attack that killed seven peacekeepers in Darfur

Remains of peacekeepers killed in ambush in South Darfur are prepared for repatriation to their home country of Tanzania. Photo: UNAMID/Saidi Msonda




13 July 2013 – Secretary-General Ban Ki-moon expressed his outrage at the attack that killed seven United Nations peacekeepers and wounded 17 military and police personnel.
In a statement, Mr. Ban's spokesperson said the Secretary-General was “outraged to learn of a deadly attack on peacekeepers […]” and said he expects the Government of Sudan will take swift action to bring the perpetrators to justice.
In a news release, the joint African Union-United Nations Mission in Darfur (UNAMID) said this morning one of its patrols was ambushed and came under heavy fire from a large unidentified group approximately 25 kilometres west of the Mission's Khor Abeche team site.
Following an extended firefight, the patrol was extracted by UNAMID reinforcements that arrived from the Mission's Khor Abeche and Manawashi sites.
Seven Tanzanian peacekeepers were killed and 17 military and police personnel, among them two female police advisers, were wounded.
Mr. Ban expressed his deepest sympathies to the families of the fallen peacekeepers, the Government of Tanzania and to all UNAMID personnel.
UNAMID Joint Special Representative Mohamed Ibn Chambas also condemned “in the strongest possible terms those responsible for this heinous attack on our peacekeepers,” and added that “the perpetrators should be on notice that they will be pursued for this crime and gross violation of international humanitarian law.”
The Security Council echoed Mr. Ban's remarks, calling on the Government of Sudan to investigate the incident and expressing deep concern at the serious nature of the attack, calling it “one of the most severe attacks on UNAMID since its deployment.”
In a statement, members of the Council underlined that any attack or threat of attack on UNAMID is unacceptable, and demanded that there be no recurrence of such attacks.
They also reiterated their full support for UNAMID and called on all parties in Darfur to cooperate fully with the Mission.
Established in July 2007, UNAMID has the protection of civilians as its core mandate. In addition, the peacekeeping operation is tasked with facilitating the delivery of humanitarian aid and assisting with an inclusive peace process in Darfur, where fighting broke out nine years ago, pitting Government forces and allied militiamen against rebel groups.

Friday, July 12, 2013

Tanzania na Kuwait zasaini Mkataba wa Ushirikiano katika masuala ya Siasa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akimkaribisha nchini Mhe. Sheikh Khalifa Al Hamad Al Sabah, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.

Mhe. Membe na Mhe. Al Sabah wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu Ushirikiano katika masuala ya Siasa kati ya Tanzania na Kuwait. Tukio hilo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Julai, 2013. Kulia ni Bw. Benedict Msuya, Afisa Mambo ya Nje.
Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Al Sabah (hayupo pichani) walipokutana. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (wa kwanza kushoto kwa Mhe. Membe), Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Prof. Abillah Omar (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto)

Mhe. Al Sabah akizungumza na Mhe. Membe (hayupo pichani).
Mhe. Al Sabah akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na Mhe. Membe.
Picha ya pamoja.

 Mhe. Membe akimpatia maelekezo Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Naimi Aziz ambaye alishiriki mazungumzo kati ya Mhe. Membe na 
Mhe. Al Sabah.


Mhe. Prof. Omar (katikati) na Balozi Yahya (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kutoka kushoto ni Bw. Abas Mngwali, Bw. Hassan Mwamweta na Bi. Tagie Daisy Mwakawago.



Picha na Ally Kondo.

Mhe. Membe amuaga Balozi wa Uholanzi hapa nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akiongea kwa msisitizo wakati wa hafla ya kumuaga Mhe. Ad Koekkoek ambaye ni Balozi wa Uholanzi aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini. Hafla hiyo  ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2013.

Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini akiwemo Mhe. Alfonso Lenhardt (kulia), Balozi wa Marekani hapa nchini.

Mhe. Balozi Koekkoek naye akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.


Wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano, Balozi Dora Msechu akizungumza machache wakati wa hafla hiyo.

Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Balozi Koekkoek wakati wa hafla ya kumuaga Balozi huyo.

Mhe. Membe akimwonesha Mhe. Balozi Koekkoek zawadi ya picha ya kuchora ya Twiga aliyomkabidhi.

Mhe. Balozi Koekkoek akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na Mhe. Membe.

Balozi Msechu akibadilishana mawazo na Mhe. Balozi Koekkoek.

Thursday, July 11, 2013

Kaimu Katibu Mkuu afungua Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Mambo ya Nje  wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) akifungua rasmi mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2013. Mkutano huo ni maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 13 Julai, 2013.

Balozi Gamaha (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Kamishina wa Magereza wa Afrika Kusini, Bw. Tom Moyane (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Usalama wa Namibia, Bw. Ben Likando (Kulia) na Mkurugenzi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Luteni Kanali Mstaafu, Tanki Mothae (kushoto) kabla ya ufunguzi wa mkutano huo.

Wajumbe wa Tanzania wakimsikiliza Balozi Gamaha (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kulia ni Mhe. Radhia Msuya, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na Balozi Naimi Aziz, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wajumbe kutoka nchi wanachama wa SADC wakimsikiliza Balozi Gamaha (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa Makatibu Wakuu.

Wajumbe wengine wakati wa ufunguzi.


Wajumbe wa Sekretarieti ya SADC.

Balozi Gamaha akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mkutano huo.    




Picha na Reginald Philip na Olga Chitanda.