Thursday, November 3, 2016

Mkurugenzi wa ushirikiano wa Kimataifa akutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy (kushoto) akifafanua jambo wakati akifanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchini Canada Mhe. Sarah Fountain Smith (kushoto) alipotembelea Wizara Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo wamezungumzia masuala mbalimbali ya kimaendeleo ya jamii na uchumi ambayo yanalenga kudumisha na kukuza uhusiano baina ya nchi hizi mbili.

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akimsikiliza Naibu Waziri wa Canada Mhe.Sarah Fountain Smith wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Wizarani Jijini Dar es Salaam

Balozi Celestine Mushy akimkabidhi kitabu Mhe. Sarah Fountain Smith
Tokea kushoto; Balozi wa Canada nchini, Mhe.Ian Myles, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Sarah Fountain Smith, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, maafisa kutoka Wizarani Bi. Ngusekela Nyerere na Bi. Lilian Kimaro  wakiwa katika picha ya pamoja.



2017 SADC SECONDARY SCHOOL ESSAY COMPETITION



Joint Communique Between Tanzania and Morocco

                        


                           
JOINT COMMUNIQUE BETWEEN THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND THE KINGDOM OF MOROCCO ISSUED AT THE CONCLUSION
OF THE STATE VISIT TO THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
BY HIS MAJESTY MOHAMMED VI, KING OF MOROCCO

1.             At the invitation of His Excellency Dr. John Pombe Joseph Magufuli, President of the United Republic of Tanzania, His Majesty Mohammed VI, King of Morocco paid a State Visit to the United Republic of Tanzania from 23rd to 25th October, 2016.  During visit, His Majesty Mohammed VI was accompanied by a high level delegation, including Ministers, Senior Officials of the Government of the Kingdom of Morocco, as well as members of the Moroccan business community.
2.             In a cordial and friendly atmosphere, the two countries have decided to work together and coordinate their respective efforts to address the challenges that Africa faces in terms of development, stability and security.
3.             President Magufuli commended the leadership of His Majesty King Mohammed VI and paid tribute to His role in promoting peace, stability and development in Africa. He recognized that the South-South cooperation advocated by His Majesty the King Mohammed VI – based on pragmatism, efficiency and public-private partnership is at the core of development cooperation in Africa.
4.             President Magufuli also paid tribute to the leading role that Morocco has been playing in promoting economic growth and sustainable development in various international fora and commended Morocco’s decision to host COP.22 meeting from 7 - 18 November 2016, in Marrakech.
5.             On bilateral issues, the two Heads of State commended the friendly relations between the two countries and committed to work together with a view to further strengthening    the bilateral relations between the two brotherly countries. They reiterated their readiness to establish an Embassy of the Kingdom of Morocco in Tanzania and a Consulate General of the United Republic of Tanzania in Morocco.
6.             In this context, they further vowed to enhance these ties of friendship of cooperation in various fields, including tourism, agriculture, railway transport, and trade. They also pledged to continue exploring new areas of cooperation, such as in economic, scientific, technical and cultural domains, as well as security cooperation and fight against terrorism and radicalism, for the mutual benefit of the two countries and peoples.
7.             To that end, they commended Tanzania-Morocco Trade and Investment Forum that was held on 22nd October 2016, which offered an opportunity for business leaders from the two countries to discuss ways and means to promote two-way trade and set up a win-win economic partnership.
8.             They also witnessed the signing of a number of Agreements and Memoranda of Understanding between both countries in the public and private sectors, covering cooperation on a wide range of areas, including political consultations, agriculture, fisheries, energy, logistics, air services, culture, science and technology, tourism, air services and finance.
9.             In order to realize the desired gains for their two peoples, the two Heads of State directed their Ministers and Senior Officials to work determinedly to implement the signed agreements between Morocco and Tanzania. It is in this spirit that His Excellency President Magufuli declared that henceforth the referral visa requirement for citizens of Morocco coming to Tanzania has been lifted.
10.         On international issues, the two Heads of State discussed the decision of Morocco to rejoin the African Union. In this respect, H.E. Dr. John Pombe Joseph Magufuli expressed Tanzania’s support to Morocco's decision to integrate and find its rightful place in the African Union. He further expressed his readiness to support the admission of Morocco to the Pan – African Institutional family as early as the next Summit.  The two Heads of State expressed their hope that the return of Morocco to the African Union would pave the way to address the longstanding political and diplomatic issues of concern to Morocco.
11.         Regarding the Sahara issue, H.E. Dr. John Pombe Joseph Magufuli expressed the support of Tanzania to the efforts by the United Nations to reach a just, lasting and mutually agreed solution. In the spirit of reconciliation and search for a lasting solution, Tanzania understands the established position of Morocco, welcomes its serious and credible Moroccan efforts and is ready to contribute towards implementation of the relevant resolutions of the United Nations on this issue.
12.         The two Heads of States share the same ambitious vision for Africa masters of its own destiny, in charge of its own development and committed to the path of stability. They underscored, in this regard, the need to strengthen South-South and triangular cooperation, and to promote a continuous and sustainable development, based on the valuation of own African resources and skills.
13.         During the visit, His Majesty Mohamed VI also unveiled the plaque for the construction of a Mosque to be erected with the gracious contribution of His Majesty the King of Morocco at the BAKWATA Headquarters in Dar es Salaam.
14.         At the conclusion of the Official Visit, His Excellency President Dr. John Pombe Joseph Magufuli expressed his profound gratitude and appreciation to His Majesty Mohammed VI for honoring his invitation and for the fruitful discussions they held. On his part, His Majesty Mohammed VI expressed his profound gratitude and appreciation to His Excellency President Dr. John Pombe Joseph Magufuli, the Government and People of the United Republic of Tanzania for the invitation extended to him as well as the warm reception and hospitality accorded to him and his delegation during the entire duration of his visit. Finally, the two Heads of State underscored their firm desire and commitment of their respective Governments to strengthen the ties of friendship and cooperation between the two countries.

           Done at Dar es Salaam, on 26th October, 2016

Wednesday, November 2, 2016

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje afungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Troika ya SADC

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Troika), Balozi Dkt. Aziz Mlima akifungua rasmi Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kutoka Asasi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupitia agenda mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kwenye Kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 03 Novemba, 2016 katika Ukumbi huo. Asasi ya SADC inaundwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania (Mwenyekiti),  Angola (Makamu Mwenyekiti) na Msumbiji (Mwenyekiti aliyemaliza). Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Mhe. Dkt. Stergomena Tax.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu. Kulia ni Balozi Mlima.
Sehemu ya Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa kikao. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi HassanYahya Simba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bw. Job Masima na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Innocent Shiyo.
Sehemu ya Ujumbe wa Msumbiji wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo


Sehemu ya ujumbe kutoka Angola wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu
Sekretarieti ya SADC
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakati wa kikao hicho cha Makatibu Wakuu

Balozi Msechu azindua zoezi la kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi

Balozi wa Tanzania katika Nchi za Nordic na Baltic mwenye makazi yake Sweden,  Mhe. Dora Msechu wa pili kutoka kulia akikata utepe kuashiria uzinduzi wa zoezi la kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera lilifanyika Stockholm, Sweden. Hafla hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Sweden kwa lengo la kuhamasisha Watanzania waishio Sweden kuchangia Wahanga wa Maafa ya tetemeko la ardhi Mkoani Kagera. Zoezi hili maalum la kuchangia maafa linaendelea mpaka tarehe 4 Novemba, 2016 na michango itakayopatikana itakabidhiwa kwa Mhe. Balozi Dora Msechu

Mhe. Balozi Dora Msechu akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania katika Mji wa Malmo ambaye aliwasilisha salaam za watanzania waishio Malmo

Sehemu ya wadau walioshiriki hafla hiyo

Mwanadiaspora Mbarouk Rashidi akikabidhi vifaa kwa Mhe.Balozi Dora Msechu

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro FC, Bw. Humphrey Kalanje akizungumza katika hafla hiyo

Tuesday, November 1, 2016

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa akutana na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kutoka Liberia

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akizungumza na Mkurugenzi wa Mipango, Maendeleo na Uratibu kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia, Bw. Theophilus Addey. Katika mazungumzo yao yalijikita katika kuelezea namna Serikali ya Tanzania inavyofanya kazi na Umoja wa Mataifa kupitia Mfumo wa One United Nations (One UN). Balozi Mushy alimweleza Bw. Addey kuwa Tanzania imekuwa nchi ya mfano wa kuigwa kutokana na mafanikio  makubwa yaliyofikiwa katika utekelezaji wa mfumo huo tangu kuanzishwa kwake hapa nchini mwaka 2007. Bw. Addey ameambatana na ujumbe wa pamoja kutoa Serikali ya Liberia na Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo.
Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Bw. Addey wafuatilia mazungumzo.
Sehemu ya Maafisa wa Mambo ya Nje nao wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mushy na Bw. Addey (hawapo pichani)
Sehemu nyingine ya Maafisa Mambo ya Nje.
Balozi Celestine Mushy akimwelezea Bw. Theophilus Addey kitabu kinachoelezea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini
Balozi Mushy akiwa katia picha ya pamoja na ujumbe wa pamoja kati ya Serikali ya Liberia na Ofisi ya Umoja wa Mataifa. 

NI MUHIMU ICC NA AFRIKA KUZUNGUMZA –TANZANIA

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipopokea na kujadili Ripoti ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC) hapo jumatatu. Katika kuchangia Ripoti hiyo, Tanzania imesisitiza haja na umuhimu kwa ICC kukaa na kuzungumza na Nchi za Afrika ili kutafuta suluhu ya misuguano baina ya pande hizo mbili.

 ****************************************************************

Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muugano wa Tanzania imeishauri Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC) kukaa meza moja na nchi wanachama wa Mkataba wa Roma hususani zile za Afrika ili kutafuta suluhu ya changamoto na tofauti zilizopo kati ya mahakama hiyo na wanachama wake.
 
Tanzania imetoa wito huo siku ya jumatatu kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lilipopokea na kujadili Taarifa ya Utendaji ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai.

Taarifa ICC imewasilishwa na Rais wa mahakama hiyo Jaji Slivia Fernandez de Gumendi katika kupindi ambacho Jumuiya ya Kimataifa imekumbwa na taharuki baada ya wanachama wawili wa Mkataba wa Roma, Afrika ya Kusini na Burundi kuwasilisha rasmi katika Umoja wa Mataifa kusudio la kujiondoa huku Gambia nayo ikitangaza kutaka kujitoa ingawa bado haijawasilisha rasmi nia yake hiyo.

Mwakilishi huyo wa Tanzania katika mchango wake amesema, uwepo au kuanzishwa kwa ICC kulitokana kwa kiasi kikubwa na uungwaji mkono kutoka Afrika. Akasema uungwaji mkono huo ulitokana hasa baada ya nchi hizo za Afrika kukatishwa tamaa na kuvunjika moyo baada ya kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

“Baada ya kukatishwa tamaa na kuvunjwa moyo, Mahakama hii, ilikuja kuwa chombo cha kutenda haki dhidi ya watu waliojihusisha na vitendo vya kikatili vikiwamo vya ukatili dhidi ya binadamu, uhalifu kivita na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Madhira yasiyoelezeka yaliyotokea Barani Afrika yakaifanya mahakama hii kuwa chombo cha matumaini dhidi ya wale ambao hawakuweza kuguswa au walikuwa juu ya sheria”. Akasema Balozi Manongi.

Tuesday, October 25, 2016

Wamisri watangaziwa fursa za Uwekezaji za hapa nchini


Mhe. Mohammed Haji  Hamza, Balozi wa Tanzania nchini Misri akiwakaribisha wageni waliohudhuria katika ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na misri lililofanyika  katika miji ya Cairo na Alexandria kuanzia tarehe 17 hadi 19 Oktoba 2016.
Kongamano hili lililowakutanisha wafanyabiashara kutoka nchi hizi mbili lilifunguliwa na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Mhe Balozi Amina Salim Ali. Kongamano hilo lilihudhuriwa na washiriki kutoka sekta mbalimbali zinahusika na uwekezaji, biashara, ujenzi, usafirishaji, elimu, afya, viwanda, uhandisi ,kilimo na utalii. Kongano hilo liligharmiwa na kuratibiwa  kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Tanzania nchini Misri, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, Jumuiya za Wafanyabiashara wa Misri na makampuni binafsi ya biashara ya Misri.
Katika kongamano hilo washiriki wa Tanzania pamoja na kutoa mada zilizohusu fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania na hasa katika sekta ya viwanda na utalii pia walipata fursa ya kushiriki katika mazungumzo  ya ana kwa ana ya kibiashara.
Siku ya pili ya kongamano hili washiriki kutoka Tanzania walipata nafasi ya kutembelea sehemu mbalimbali za uzalishaji na huduma zikiwemo: kijiji cha teknolojia cha Cairo, viwanda vya utengezaji madawa, vifaa tiba na rangi za ujenzi mjini Cairo pamoja na viwanda vya nguo, vifaa vya ujezi na samani za chuma katika miji wa Tenth Ramadhani .  Siku ya tatu ya kongamano hilo baadhi ya washiriki kutoka Tanzania walitembelea vyuo vikuu vya Alexandria na chuo kikuu cha kiarabu cha sayansi, teknolojia na usafiri wa bahari mjini Alexandria na kuwa na mazungumzo ya ushirikiano na viongozi wa vyuo vikuu hivyo. Ujumbe wa Tanzania pia ulipata nafasi ya kutembelea kiwanda cha kutengenezea manukato kilichopo nje kidogo ya jiji la Akexandria.

Akiwa jijini Cairo, Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika kongamano hilo alipata nafasi ya kukutana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri, Rais na Mtendaji Mkuu wa  Afri exim bank na Katibu Mkuu wa Wakala wa Ushirikiano na Maendeleo wa Misri.. 

Vingozi mbalimbali walioshiriki kwenye ufunguzi wa konganano la kibiashara mjini Cairo siku ya  tarehe 17 Oktoba 2016 wakisimama wakati wa Nyimbo za Taifa za Tanzania na Misri zilipopigwa. Wa kwanza kutokea kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda wa Misri. Wa pili ni Katibu Mkuu wa Wakala wa Ushirikiano na Maendeleo wa Misri, watatu ni Mhe Balozi Amina Salim Ali, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Mohamed Haji Hamza , watano ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar na wa sita ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Biashara ya Misri. Waliosimama mbele ya meza kuu ni Mabalozi kutoka nchi za  SADC waliopo mjini Cairo.

Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Zanzibar akifuatilia neno la ukaribisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Mohammed Haji Hamza
Balozi Hamza akisalimiana na kubadilishana mawazo na washiriki mbalimbali wa kongamano la biashara jijini Cairo mara baada ya ufunguzi kukamilika.

Monday, October 24, 2016

Waziri Mahiga ahimiza umuhimu wa somo la Umoja wa Mataifa

WAZIRI MAHIGA AHIMIZA UMUHIMU WA SOMO LA UMOJA WA MATAIFA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine mahiga amependekeza ni vema somo la Umoja wa Mataifa likaingizwa katika mitaala ya masomo, ameeleza hayo alipokuwa akihutubia  katika kilele cha Maadhimisho ya 71 ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo Waziri Mahiga alisema “Maadhimisho haya ni muhimu  kwa historia ya nchi yetu kwakua yanawezesha vizazi vyetu kuelewa historia ya nchi yetu na Shirika la Umoja wa Mataifa tangu kupatikana kwa Uhuru hivyo ni vyema Walimu na Wadau wote katika Sekta ya Elimu wakatilia mkazo umuhimu wa somo la Umoja wa Mataifa katika shule zetu za Msingi na Sekondari.”

Vilevile ameeleza umuhimu na mchango wa Shirika la Umoja wa Mataifa kwa Tanzania na  kwa nchi wanachama wengine wa Umoja huo ni pamoja na kutengeneza agenda ya kimataifa ya maendeleo; kuleta amani hususan baada ya vita ya kwanza na  ya pili ya Dunia; vilevile Shirika hilo limekuwa likiendelea kuhakikisha amani na Ulinzi inapatikana katika mataifa yenye migogoro ambapo Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimekuwa zikishiriki katika masuala ya ulinzi wa amani katika baadhi ya mataifa kama Lebanon, Sudan Kusini (Dafur) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Pamoja na hayo ameeleza kuwa kupitia shirika la umoja wa Mataifa Tanzania imefanikiwa kuwa na  wawakilishi wa mashirika yote ya Umoja wa Mataifa ambao pamoja na shughuli nyingine za mashirika hayo yamekuwa yakifadhili na kushiriki katika shughuli za maendeleo ambapo wastani wa bilioni za fedha za miradi ya maendeleo zimekuwa zikitolewa kwaajili ya miradi ya maendeleo. Vilevile Mahakama ya Umoja wa mataifa ya mauaji ya kimbari iliamuriwa kujengwa nchini Tanzania ambapo makao makuu yake yapo Jijini Arusha licha ya kumalizika kwa kesi majengo pamoja na nyaraka zote zilizokuwa zikitumika zimeendelea kubaki nchini kama kumbukumbu za marejeo.

Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez alieleza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs), umuhimu wa kutunza amani na kuheshimu haki za binadamu sambamba na usawa wa jinsia.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa yanayowakilisha nchi zao hapa nchini. Wengine ni wadau wa maendeleo kutoka Sekta binafsi na taasisi za Serikali. 


Mfalme wa Morocco aendelea na ziara nchini

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI 



Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

                20 KIVUKONI FRONT,
                           P.O. BOX 9000,
             11466 DAR  ES SALAAM, 
                                    Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MFALME WA MOROCCO AENDELEA NA ZIARA NCHINI

Mfalme wa Morocco, Mtukufu Mohammed VI aliyewasili jana kwa ziara ya kitaifa, ameendelea na ziara yake nchini ambapo leo alifanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijikita zaidi katika kuboresha mahusiano ya Tanzania na Morocco katika maeneo mbalimbali ya Kidiplomasia, Siasa, Uchumi, Ulinzi na Ustawi wa Jamii.

Akielezea mahusiano ya Tanzania na Morocco, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) alisema kuwa ziara hii ni matokeo ya  Mhe. Rais kuridhia ujio huo wa Mfalme wa Morocco na ujio wake umekuwa ni maalum sana kwa kuwa unakumbushia historia iliyowekwa na mgeni wa kwanza kutoka Morocco, Bw. Iban Batutu aliyetembelea Tanzania eneo la Kilwa Mwaka 1631.

Baada ya mazungumzo,  Mhe. Rais Magufuli na Mgeni wake, Mtukufu Mfalme wa Morocco walishuhudia uwekaji saini wa Mikataba 22 ambayo inalenga kuendeleza sekta mbalimbali kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Morocco.

Baadhi ya Mikataba hiyo ni Makubaliano baina ya Benki ya Kilimo ya Tanzania na Benki ya Kilimo ya Morocco  ili kuwawezesha wakulima wetu kusindika mazao yao na kuyasafarisha nje yakiwa yamekamilika, Makubaliano baina ya Kampuni ya Mbolea ya Morocco na ya Tanzania ambapo kwa pamoja zitabadilishana uzoefu na utaalamu kwa lengo la kuiwezesha kampuni ya Tanzania kuzalisha mbolea ya kutosha kulingana na mahitaji, Makubaliano katika Sekta ya Anga ambapo katika siku za usoni Shirika la Ndege la Morocco litaanzisha usafiri wa moja kwa moja kutoka Rabat hadi Dar es Salaam.

 Makubaliano mengine ni pamoja na kusaidia wakulima wadogo wadogo, kuendeleza Sekta ya Utalii ya Tanzania hususan katika fukwe za Zanzibar na hifadhi za Taifa za Serengeti na Ngorongoro, makubaliano  baina ya Shirika la reli la Tanzania na lile la Morocco ambapo watashirikiana  kuboresha usafiri  wa reli kwa madhumuni ya kupunguza gharama za uzalishaji pamoja na kuendeleza reli ya Mtwara-Mchuchuma/Liganga.

Viongozi hao pia walishuhudia uwekaji saini ya Mkataba baina ya Kampuni ya chai ya Tanzania na ile ya Morocco kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali kutengeneza chai yenye ubora wa hali ya juu ili iweze kupata soko nchini Morocco na nchi nyingine.

Aidha, akiongea katika mazungumzo hayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Salahddine Mezouar amesema wakati sasa umefika nchi hizi kupeleka mbele mahusiano yao na hii ndio sababu kubwa iliyopelekea nchi hizi mbili kukubaliana kusaini jumla ya mikataba 22, amesema nchi ya Morocco imefurahishwa na utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuri.

Mtukufu Mfalme atahitimisha ratiba yake kwa siku ya leo kwa kushiriki dhifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli  Ikulu, Dar es Salaam.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 24 Septemba 2016

Rais Magufuli ampokea Mfalme Mohammed VI wa Morocco Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco wakipungia mikono wananchi waliojitokeza kwenye mapokezi ya Mfalme huyo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Mfalme Mohammed VI wa Morocco akisalimia wananchi waliojitokeza kumpokea Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya Mfalme huyo kuwasilia Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mfalme Mohammed VI wa Morocco wakiwa katika Mazungumzo, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza katika hafla ya kutoa taarifa ya mazungumzo maalum, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika hafla ya kutoa taarifa ya mazungumzo maalum, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Tanzania yaungana na Nchi zingine Duniani kuadhimisha kilele cha Siku ya Umoja wa Mataifa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na watendaji wa mashirika mbalimbali ya Kimataifa yaliyopo Nchini kwenye maadhimisho ya kilele cha Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa amesimama sehemu maalumu wakati wimbo wa taifa ukipigwa
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akikagua gwaride maalum katika maadhimisho  ya kilele ya Siku ya Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria maadhimisho ya Kilele ya Umoja wa Mataifa
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia kwenye maadhimisho ya kilele ya Siku ya Umoja wa Mataifa 
Baadhi ya wanafunzi wenyemahitaji maalum wakiwa wameshikilia mabango ya malengo 17 ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa