Saturday, September 28, 2019

TAMASHA LA JAMAFEST LAMALIZIKA KWA MAFANIKIO

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akitoa hotuba ya kufunga rasmi Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST ) lililofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28 Septemba 2019. Tamasha hilo la aina yake lilizishirikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania. Wakati wa Tamasha hilo vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni kutoka nchi hizo vilishiriki. Katika hotuba yake Mhe. Balozi Iddi alitoa rai wadau wa sanaa na utamaduni kujikita kwenye ubunifu kwa ajili ya kukuza uchumi kupitia sanaa. Tamasha la JAMAFEST ambalo hufanyika kila baada ya miaka miwili limepangwa kufanyika mwaka 2021 nchini Burundi
Mhe. Balozi Iddi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Christopher Bazivamo alipowasili kwenye Tamasha la JAMAFEST
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akifuatilia hotuba ya Mhe. Balozi Iddi (hayupo pichani)

Sehemu ya wageni waalikwa wakiwemo viongozi wa dini wakiwa kwenye sherehe za ufungaji wa Tamasha la JAMAFEST
Sehemu nyingine ya wageni waalikwa

Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akipata maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki kuhusu Banda la Maonesho la Wizara hiyo  alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho yaliyofanyika wakati wa Tamasha la JAMAFEST
Mhe. Balozi Iddi akipata maelezo kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii
Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimsikiliza mmoja wa washiriki wa maonesho alipotembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii
Mhe. Balozi Iddi akiwa kwenye banda la Zanzibar
Mhe. Balozi Iddi akiwa kwenye Banda la Rwanda

 

Mhe. Balozi Iddi akiwa kwenye banda la Burundi

Mhe. Balozi Iddi akiwa kwenye banda la Uganda

Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza wakati wa sherehe za kuhitimisha Tamasha la JAMAFEST
Wasanii kwenye JAMAFEST

Watoto kutoka Dodoma wakitumbuiza

PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI AHUTUBIA KATIKA MKUTANO MKUU WA 74 WA BARAZA LA UMOJA WA MATAIFA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akihutubia katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akihutubia katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika ukumbi wa Umoja wa Mataifa muda muchache kabla ya hutubia katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. Kulia ni Waziri wa Afya wa Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohamed akifuati na Waziri wa nchi,Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na nyuma ya Prof. Kabudi ni Balozi Ali Abeid Amani Karume. 

Ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Mataifa kunaofanyika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliopo New York,Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (mwenye tai nyekundu katikati) akiwa katika  picha ya pamoja na baadhi ya viongozi muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia katika Mkutano Mkuu wa 74 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa,New York Marekani.

Baadhi ya viongozi na watumishi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia katika mkutano mkuu wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York,Marekani.



Thursday, September 26, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA WHO NEW YORK MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa pamoja na Dkt. Tedross Adhamon Ghebreyesus,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kulia ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mero. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa katika mazungumzo na Dkt. Tedross Adhamon Ghebreyesus,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).Mazungumzo hayo yamefanyika New York, Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiagana na  Dkt. Tedross Adhamon Ghebreyesus,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) mara baada ya kumaliza mazungumzo walipokutana Jijini New York Nchini Marekani.


Wednesday, September 25, 2019

PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI KATIKA PICHA YA PAMOJA NA RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP NA MKEWE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Marekani Donald Trump na Mkewe Melania. Prof. Palamagamba John Kabudi yuko New York Marekani kuhudhuria mutano wa 74 wa Baraza la Umoja wa Mataifa.

TANZANIA KUNUFAIKA NA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 120 KUPAMBANA NA SELI MUNDU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett Giroir. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani.

Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett Giroir akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo Pichani) wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett Giroir. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika  
Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika  Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

MAREKANI KUTOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 120 KUPANDA NA UGONJWA WA SELI MUNDU (SICKLE CELL)

Tanzania ni miongoni mwa baadhi ya Nchi zinazotarajiwa kunufaika na kiasi cha dola za Kimarekani milioni 120 zilizotengwa na Serikali ya Marekani kwa ajili ya utafiti wa kupambana na ugonjwa wa  seli mundi (sickle cell).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett Giroir wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi jijini New York Nchini Marekani.

Admiral Brett ameutaja mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi kama mwanzo mpya wa ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani na kuongeza kuwa Nchi yake ina nyenzo zote ikiwemo teknolojia ya kuoambana na maradhi ya seli mundu ili kuboresha Maisha ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo.

Ameongeza kuwa katika siku za hivi karibuni Tanzania imekuwa ikipiga hatua chanya katika kuimarisha masuala mbalimbali ya afya za wananchi wake na kwamba ni azma ya Marekani kuona kuwa ugonjwa wa seli mundo unapata tiba.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema utafiti na hatimae tiba ya maradhi hayo ya seli mundu kwa kiasi kikubwa itainufaisha Tanzania kutokana na kushika nafasi ya tatu katika Bara la Afrika na ya nne duniani kwa kuwa na wagonjwa wengi wa seli Mundu.

Ameongeza kuwa Tanzania na Marekani zitashirikiana katika kufundisha na kujengeana uwezo wa namna ya kupambana na maradhi ya seli mundu lakini pia kutafuta fedha zitakazowezesha upatikanaji wa dawa ya seli mundu kutokana na ukweli kuwa dawa za ugonjwa huo kwa Tanzania ni miongoni mwa dawa muhimu yaani essential drugs ili iweze kuwafikia wananchi wengi na kwa bei nafuu.

Amezitaja Nchi zilizo na idadi ya watoto wengi wanaozaliwa na ugonjwa wa seli mundu ambapo kwa Afrika Tanzania ni ya tatu baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Nigeria nay a nne duniani baada ya India.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
New York,Marekani
25 Septemba 2019

Tuesday, September 24, 2019

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA TAMASHA LA JAMAFEST LINALOENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akitoa mchango wake wakati wa warsha kuhusu namna utamaduni unavyochangia uchumi na maendeleo ya nchi za kanda ya Afrika Mashariki na namna ya kutangaza utalii kupitia sanaa na utamaduni iliyofanyika sambasamba na Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama JAMAFEST linaloendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ambalo lilifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais tarehe 22 Septemba 2019 linatarajiwa kumalizika tarehe 28 Septemab 2019. 
Watoa mada na wachangiaji wakiwa kwenye warsha hiyo iliyojadili kwa kina masuala ya mila na tamaduni zinavyoweza kuchangia uchumi wa nchi za Afrika Mashariki
Sehemu ya washiriki wa warsha 
Washiriki wakifuatilia mada zilizowasilishwa kwenye warsha hiyo
Sehemu nyingine ya washiriki
Wanafunzi nao wakishriki warsha hiyo iliyojadili masuala kuhusu Utamaduni
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Dkt. Harrison Mwakyembe akipata maelezo kutoka kwa washiriki wa maonesho ya bidhaa zinazotengenezwa kwa mikono wakati wa tamasha la JAMAFEST linaloendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Washiriki wa maonesho ya bidhaa mbalimbali za utamaduni wakiwa kwenye mabanda yao wakati wa Tamasha la JAMAFEST 2019
Sanaa za Utamaduni kama zinavyoonekana kwenye  Tamasha la JAMAFEST
Vinyago katika banda mojawapo la Tanzania
Sanaa za maonesho kama zinavyoonekana

PROF. KABUDI AMUWAKILISHA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI UNGA


  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akifuatilia Mkutano wa viongozi wa ngazi ya juu kuhusu upatikanaji wa huduma za afya kwa wote ambao unafanyika sambamba na mkutano wa 74 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa New York, Marekani.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika Mkutano wa viongozi wa ngazi ya juu kuhusu upatikanaji wa huduma za afya kwa wote ambao unafanyika sambamba na mkutano wa 74 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa New York, Marekani.


 Baadhi ya wajumbe wanaoshiriki katika Mkutano wa viongozi wa ngazi ya juu kuhusu upatikanaji wa huduma za afya kwa wote ambao unafanyika sambamba na mkutano wa 74 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa New York, Marekani. Katika Mkutano huo Tanzania inawakilishwa na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)


NAIBU WAZIRI DKT DAMAS NDUMBARO AMUAGA BALOZI WA QATAR NCHINI TANZANIA

Balozi wa Qatar nchini Tanzania,Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi akibadilishana nyaraka na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro wakati alipomtembelea Naibu Waziri kwa lengo la kumuaga katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro akiongea na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi wakati alipowasili katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Qatar.  




NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AMUAGA BALOZI WA QATAR NCHINI TANZANIA.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemuaga Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi ambaye amemaliza muda wake, na kuahidiana kudumisha mahusiano ya kidiplomasia na biashara.

Akiongea wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Qaatar ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini, Dkt. Ndumbaro amemshukuru Balozi Al-Madadadi kwa kumaliza muda wake wa uwakilishi vizuri na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda katika kipindi chake cha uwakilishi. 

Nae Balozi wa Qatar amemwambia Dkt. Ndumbaro kuwa "Nchi za Tanzania na Qatar zitaendelea kudumisha siyo tu mahusiano ya kidiplomasia bali kushirikiana katika sekta ya biashara na kukuza uchumi wa nchi zote mbili" 

Mhe. Balozi ameeleza kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi yake na Tanzania na kupongeza hatua mbalimbali ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kuzichukua katika kuimarisha mahusiano hayo.   

Monday, September 23, 2019

PROF. KABUDI ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI UNAOENDELEA NEW YORK - MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu mabadiliko ya tabianchi unaofanyika wakati wa kikao cha 74 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa New York, Marekani. Mbali kulia kwa Waziri Kabudi ni Rais wa Marekani Mhe. Donald Trump akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mhe. Mike Pompeo. Wengine ni Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) Mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu ulinzi na usalama na Balozi na mwakilishi  wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mero.