Maonesho hayo ambayo yanaratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma yatafunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Rosemary Senyamule tarehe
07 Machi 2024.
Huduma zitakazotolewa katika Banda la Wizara wakati wa maonesho hayo ni pamoja
na uthibitishaji wa nyaraka mbalimbali ikiwemo vyeti vya taaluma, ndoa na
nyaraka nyingine, zoezi ambalo litaanza rasmi tarehe 07 hadi 11 Machi, 2024.
Taarifa nyingine ni kuhusu utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje na
mchango wa wanawake kwenye medani za kimataifa na diplomasia.
Kadhalika maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim zamani Chuo cha Diplomasia; Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) na Mpango wa Hiari wa Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) yatatolewa.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2024 yamebeba kaulimbiu
isemayo "Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa
Jamii".
Afisa kutoka Taasisi ya Wizara ya Mpango wa Hiari wa Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM), Bi. Praxeda Gaspar akimpatia Bw. Kawina kipeperushi kuhusu Taasisi hiyo |
Bw. Kawina akipata maelezo kutoka kwa Bi. Janeth Benedict kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) kuhusu vipeperushi watakavyosambaza kwa wananchi kuhusu taasisi hiyo |
Mwonekano wa Banda la Wizara |