Friday, October 24, 2014

Sherehe za kuadhimisha miaka 69 UN zafana.

Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee huku akiwa ameongozana Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Pichani juu na chini ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimtambulisha mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka kwa baadhi ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akipokea heshima ya wimbo wa taifa kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe za maadhimisho miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akipokea heshima ya wimbo wa taifa kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe za maadhimisho miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mabalozi nchini na ni Balozi wa Kongo nchini Tanzania, Balozi Juma Mpango, na katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajab Gamah, na wakwanza kulia ni Brigadia Jeneral Dominic Basil Mrope wa JWTZ wakiwa wamesimama wakati Mgeni rasmi akikagua gwaride. 
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akikagua gwaride maalum kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika leo jijini Dar
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akisoma risala kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Mambo ya Nje Balozi Celestine Mushy akimpongeza Mhe. Waziri Tibaijuka mara baada ya kumaliza kusoma hotuba yake.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Wageni mbalimbali wakisikiliza hutoba ya Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez


Mshehereshaji wa sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa Maulida Hassan kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa mwongo wa hotuba mbalimbali kwa meza kuu.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akishuhudia bendera ya Umoja wa Mataifa ikipandishwa kama ishara ya kuadhimisha miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Umoja Mataifa (UNA), Bw. Benedict Kikove akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Viongozi mbalimbali wa Jeshi wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa 
Kikundi cha watoto walemavu wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya miaka 69 ya UN
Viongozi walioko meza kuu wakiwapongeza watoto hao walipo kuwa wakionyesha onyesho lao.
Wadau kutoka Mambo ya Nje nao walikuwepo.


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.