Hon. Mahadhi and Ambassador Naimi listening to ongoing discussions during an emergency meetingon Ebola outbreak held in Addis Ababa. |
Tuesday, September 9, 2014
AU EXECUTIVE COUNCIL MEETS IN ADDIS ABABA ON EBOLA OUTBREAK
Monday, September 8, 2014
Waziri Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Mabalozi wapya wa Rwanda na Norway hapa nchini
Balozi Kayihura akiwa na Maafisa Waandamizi wa Ubalozi wa Rwanda hapa nchini aliofutana nao. Katikati ni Bw. Sano Lambert na Bw. Ernest Bugingo. |
Mhe. Membe akimsikiliza Balozi Kayihura wakati wa mazungumzo yao. |
Mhe. Membe akiagana na Balozi Kayihura..................Mhe. Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Norway nchini |
Balozi Kaarstad na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani) |
Mhe. Membe akiagana na Balozi Kaarstad. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, anatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatano asubuhi, tarehe 10 Septemba, 2014 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Katika ziara hiyo nchini, Mhe. Museveni atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam. Rais Museveni ataondoka baadaye siku hiyo hiyo kurejea nyumbani.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
|
Waziri Membe apokea Hati za Utambulisho za Mratibu Mkazi mpya wa UN nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Hati za Utambulisho za Mratibu Mkazi mpya wa Umoja wa Matiafa hapa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Membe tarehe 08 Septemba, 2014. |
Mhe. Membe akizungumza na Bw. Rodriguez mara baada ya kupokea Hatiza ke za Utambulisho. ambapo alimhakikishia ushirikiano. |
Bw. Rodriguez pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (katikati) na Bi. Hoyce Temu, Afisa kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) |
Mhe. Membe akiagana na Bw. Rodriguez mara baada ya mazungumzo yao. |
Katibu Mkuu akutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ireland
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ireland, Bw. Niall Burges mara baada ya kukutana kwa mazungumzo. Bw. alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne. |
Bw. Haule na Bw. Burges wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ireland hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan |
Bw. Haule, Bw. Burges na Mhe. Gilsenan wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Idara za Ushirikiano wa Kimataifa na Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza kushoto) na Balozi Joseph Sokoine (wa kwanza kulia) |
Wednesday, September 3, 2014
Naibu katibu Mkuu ashiriki hafla ya miaka 69 ya Taifa la Vietnam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akisoma hotuba wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Septemba, 2014 na kuhudhuriwa na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wageni waalikwa. |
Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vo Thanh Nam (kushoto) akiwa na Balozi wa Cuba nchini. Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo (wa tatu kushoto) pamoja na Bi. Samira Diria (wa kwanza kulia), Afisa Mambo ya Nje wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam. |
Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Zakaria Anshar (kushoto) akiwa na Bw. Emmanuel Luangisa (katikati), Afisa Mambo ya Nje pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Vietnam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam. |
Sehemu ya Wageni waalikwa wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakimsikiliza Balozi Gahama akihutubia wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam |
Kaimu Murugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Nathaniel Kaaya akimpongeza Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vo Thanh Nam kwa miaka 69 ya uhuru wa taifa lake. Picha na Reginald Philip |
Tuesday, September 2, 2014
Press Release
H.E. Truong Tan Sang, President of Vietnam |
PRESS RELEASE
H.E Jakaya Mrisho Kikwete,
President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message
to His Excellency Truong Tan Sang,
President of the Socialist Republic of Vietnam.
The
message reads as follows:-
“Excellency
Truong Tan Sang,
President,
Socialist Republic of Vietnam
HANOI.
Your Excellency and Dear Brother,
On
the auspicious occasion of the 69th anniversary of the National Day
of the Socialist Republic of Vietnam, the Government and the People of the
United Republic of Tanzania join me in extending to you and through you to the
Government and People of the Socialist Republic of Vietnam our heartfelt and
sincere congratulations.
Tanzania
and Vietnam have since the establishment of diplomatic relations demonstrated
close friendship and solidarity in different spheres and supported each other
at different international for a. Tanzania is determined to keep and further strengthen
this relationship in the years ahead.
Please
accept, Your Excelency and Dear Brother, the assurances of my highest
consideration along with my personal best wishes for your continued good health
and happiness as well as the progress and the prosperity of the people of
Vietnam”.
Issued by the Ministry of Foreign Affairs and
International Cooperation, Dar es Salaam
02nd September 2014
Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akutana na uongozi wa juu wa Hospital ya Iran ya Dubai
Mhe. Omar Mjenga akiwa katika
picha ya pamoja na mwenyeji wake Dk. Asghar Fashad.
|
Mhe. Omar Mjenga akizungumza na Uongozi wa Juu wa
Hospitali ya Iran, akiwemo Mkurugenzi Mkuu Dk. Asghar Fashad.
|
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Iran Dkt. Asghar Fashad akizungumza. ===========================================
Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa
Tanzania- Dubai, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa
Hospitali ya Iran ya Dubai, Dr. Asghar Fashad. Katika mazungumzo, Mhe. Mjenga
alimuomba Dr asghar kuangalia uwezekano wa kuwa na makubaliano kati ya
hospitali yake na Ubalozi Mdogo kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa
Watanzania kwa gharama nafuu ukilinganisha na gharama zake za sasa.
Baada ya mazungumzo na mashauriano ya
muda wa saa moja, Uongozi wa Juu wa Hospitali, ulikubali ombi la Mhe. Mjenga la
kupunguza gharama za matibabu kwa Watanzania kwa asilimia 40 (40%). Mwanzo,
Uongozi ulipendekeza asilimia 20, ambayo Mhe. Mjenga aliwaeleza kuwa bado
ilikuwa ni punguzo dogo na bado ingekuwa ni mzigo mkubwa kwa Watanzania.
Hatmaye, ndio maafikiano hayo yakafikiwa ya asilimia 40.
Mpango wa huu utajumuisha Watanzania
wote waishiyo UAE na wale wanaoishi nje ya UAE ikiwa ni pamoja na wale
wanaoishi Tanzania. Hospital ya Irani ni moja ya hospitali zenye huduma za hali
ya juu kwa hapa Dubai na UAE kwa ujumla.
Uongozi wa Hospitali umekubali kuanza
kutoa Vitambulisho Maalum kwa ajili ya Watanzania wote kuanzia Jumapili tarehe
1 Septemba. Mkataba wa Makubaliano haya utatiwa saini Jumatatu tarehe 2
Septemba.
Aidha, Mhe. Mjenga, amemuomba
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hii, kuangalia uwezekano wa kujenga Hospitali
kubwa yenye hadhi kama hii, nchini Tanzania. Kimsingi, Mkurugenzi Mkuu
amekubali ombi hili, na ameahidi kumuomba Rais wa Hospitali kufanya ziara
nchini Tanzania mwezi ujao ili kuona na uongozi husika na kuanza mazungumzo ya
kuanzisha Hospitali kama hiyo. Ameeleza kuwa Tanzania na Iran na nchi marafiki
wa siku nyingi, na hivyo Iran inafarijika sana kuwa karibu na Tanzania
kimahusiano.
|
Monday, September 1, 2014
Mhe. Omar Mjenga akutana na Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce
Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai Mhe. Omar Mjenga akutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Hamad Buamim, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry. ----------------------------------------------------------------------- Mhe. Omar Mjenga, amekutana na Mhe. Hamad Buamim, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry na kufanya naye mazungumzo. Katika mazungumzo, wamejadiliana uwezekano wa kuwa na ziara ya kibiashara kwenda Tanzania, kwa makampuni na viwanda vilivyopo Dubai, ili kukutana na wafantabiashara na wamilikiwa viwanda Tanzania, ilikujionea na kuibua furs za uwekezaji. Wamekubaliana ziara hiyo ifanyike mwanzoni mwa mwaka kesho na hivyo basi kuanza maandalizi mapema Mwezi Novemba, kutakuwa na ziara ya kibiashara ya makampuni kutoka Flame ya Ajman. Aidha, wamezungumzia kuhusu mkutano wa Africa Global Business Forum utakaofanyika tarehe 1 - 2 Oktoba 2014 hapa Dubai. Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum amemwalika Rais Kikwete kuhudhuria pamoja na marais wengine wa Mali, Ghana, Uganda, Mozambique, Ethiopia, Senegal, Burkina Faso, Sudan na Ivory Coast. Mkutano huu hufanyika kila mwaka ambao huzungumzia njia muafaka wa ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na UAE kwa ujumla na nchi za Afrika. |
Saturday, August 30, 2014
Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa E- Government na Ujumbe wake wa mtembelea Balozi wetu Mdogo Dubai
Mhe. Omar Mjenga,
Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akisalimiana na Dkt.Jabir Bakari, Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa e-Government pamoja na ujumbe wake wakitokea New Delhi ambako
walikuwa na mkutano na Wakala wenzao wa Serikali ya India. Katika mazungumzo
yao, wamezungumzia jinsi ya kupata ufadhili kwaajili ya kujenga uwezo wa Wakala
wa Serikali kwa njia ya Mtandao(e- Government)
|
Picha ya pamoja |
Friday, August 29, 2014
Mhe. Omar Mjenga akutana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai
Mhe. Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Lootah mbele ya baadhi ya miradi inayojengwa na Nakheel. |
Mhe. Mjenga akifanya mazungumzo kati Mwenyekiti Lootah, katika ofisi za Nakheel.
Mhe. Omar Mjenga akutana na Mwenyekiti
wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai (NAKHEEL) Bwa. Rashid Lootah.
Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai, mhe.
Omar Mjenga, leo amemtembelea na kufanya mazungumzo na Bw. Rashid Lootah,
Mwenyekiti wa Nakheel, Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai.
Katika mazungumzo yao, wamezungumzia
ziara ya Mwenyekiti huyo pamoja na ujumbe wake kuitembelea Tanzania,
itakayofanyika kuanzi tarehe 16-20 Septemba, ambako anatarajia pamoja na
kuonana na baadhi viongozi wa Serikali, watafanya mazungumzo na Shirika la
Nyumba la Taifa(NHC) yatakayowezesha kusainiwa makubaliano ya ushirikiano kwenye
sekta ya nyumba kati ya mashirika hayo mawili.
Aidha, watapata fursa ya kukitembelea
kituo cha uwekezaji - TIC ili kupata taarifa muhimu za uwekezaji.
Aidha, Mhe. Mjenga amemuomba Mwenyekiti
huyo kufadhili mkutano wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Utalii utakaofanyika
Novemba hapa Dubai. Mkutano huo unaandaliwa na Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana
na Bodi ya Utalii ya Tanzania-TTB pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan afanya ziara nchini
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Japan Mhe. Hirotaka Ishihara mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini. Katika ziara hiyo Mhe. Ishihara amembatana na ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Japan.Anayeshuhudia katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Nathaniel Kaaya. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. hAULE pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Ishihara wakimsikiliza Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaki Okada alipokuwa akiwaeleza jambo mara baada ya mapokezi ya Mhe. Ishihara.
Picha na Reginald Philip.
|
Thursday, August 28, 2014
Ziara ya Mhe. Naibu Waziri nchini Singapore
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wa Mkutano wa
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Mhe.
Kasiviswanathan Shanmugam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore.
|
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (wa pili kushoto), Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye picha ya pamoja
na Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore (wa tatu
kushoto), Balozi Mbelwa Kairuki (kulia) na Mhe. John Kijazi (kushoto), Balozi wa Tanzania nchini
India na Singapore.
|
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na
Mawaziri saba wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wakiwa na
mwenyeji wa Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore
Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam (wa tano kutoka kushoto).
|
Mawaziri wa Mambo ya Nje wakiwa kwenye ziara kwenye mojawapo ya vyuo maalum nchini Singapore Institute of Technical Education ambapo Tanzania inashirikiana nacho kwenye kutoa mafunzo kwa walimu wa VETA. |
....Ufunguzi wa Ubalozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kushoto) akikata utepe kufungua rasmi ofisi za Ubalozi wa Heshima za Tanzania nchini Singapore akishirikiana na Mhe. S.S. Teo, Balozi wa Heshima. Kulia ni Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Singapore. |
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. John Kijazi (wa kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini India ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Singapore, Mhe.S.S. Teo, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore na Balozi Mbelwa Kairuki, Murugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa |
Waziri Nagu asaini Kitabu cha Maombolezo Ubalozi wa Ireland
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Mb) akisalimiana na Balozi wa Ireland, Mhe. Fionnuala Gilsenan mara baada ya kuwasili kwenye Ubalozi wa nchi hiyo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Ireland, Hayati Albert Reynolds kilichotokea tarehe 21 Agosti, 2014. |
Mhe. Dkt. Nagu (Mb) akisaini kitabu hicho cha maombolezo huku Balozi Gilsenan akishuhudia. |
Mhe. Dkt. Nagu na Balozi Gilsenan wakiwa katika mazungumzo.
Picha na Reginald Philip
|
President Shein meets new UNFPA Country Representative
President of the Revolutionary Government of Zanzibar, H.E. Dr. Ali Mohammed Shein welcomes Dr. Nathalia Kanem, a new Country Representative of United Nations Population Fund (UNFPA) at the State House in Zanzibar when she paid a courtesy call on Wednesday 27th August, 2014. |
H.E. President Shein shake hands with the Director of Multilateral Cooperation Department in the Ministry of Foreign Affairs and International and Cooperation, Ammbassador Celestine Mushy during their visit with Dr. Kanem to the State House in Zanzibar. |
H.E. President Shein welcomes one of UNFPA Senior Officials who accompanied Dr. Kanem. |
H.E President Shein in a discussion with Dr. Kanem and her team during their meeting at the State House in Zanzibar. |
H.E. President Shein gives a present to Dr. Kanem during her visit to the State House in Zanzibar. |
Wednesday, August 27, 2014
ANNOUNCEMENT FOR NOMINATION OF CANDIDATES FOR MEDIATION TEAM
ANNOUNCEMENT FOR NOMINATION OF CANDIDATES FOR THE DEPARTMENT OF POLITICAL AFFAIRS’ STANDBY TEAM OF MEDIATION AT THE UNITED NATIONS SECRETARIAT.
We wish to inform the
general public that the United Nations Secretariat, through the Department of
Political Affairs (DPA) is seeking the nomination of candidates for the 2015
Standby Team of Mediation Experts to undertake mediation assignments effective
from February 2015, for a one-year term.
The Team once
duly constituted will be composed of eight experts whose work shall concentrate
on the following thematic areas: (1) constitutional-making; (2) natural
resources; (3) power-sharing arrangements; (4) gender and inclusion issues; (5)
security arrangements; and (6) mediation and dialogue process design (three
positions).
Please note
that member of the Team are engaged on a full-time basis with the DPA, and
deploy on short notice to the field in support of ongoing good offices and
mediation work. In between deployments, the experts carry out research and
analysis on mediation issues, as defined by DPA.
The deadline
for submission of nomination (including the full name, title, contact details
and resumes of the nominees) is 14 September 2014. Nomination of women with knowledge of French and Arabic languages
is highly encouraged. Supplementary information about the Standby Team of Mediation
may be retrieved from the following site: http://peacemaker.un.org/mediation-support/stand-by-team.
Subscribe to:
Posts (Atom)