|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Bw. Ahmed Salim mtoto wa Dkt. Salim Ahmed Salim ambaye alikabidhiwa na Serikali ya China ikiwa ni ishara ya kuutambua mchango wa Dkt. Salim ulioiwezesha China kurejesha kiti cha Kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 1971 |
|
|
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
(kushoto) akizungumza na Bw. Ahmed Salim (katikati) mtoto wa Dkt. Salim
Ahmed Salim ambaye alifika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kumkabidhi zawadi ya picha iliyotolewa na Serikali ya China ikiwa ni ishara ya
kutambua mchango wa Dkt. Salim ulioiwezesha China kurejesha kiti cha
Kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 1971 |
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb)
amepokea zawadi ya picha
kutoka Serikali ya China ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa Dkt. Salim Ahmed
Salim ulioiwezesha nchi hiyo kurejesha kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa mwaka 1971.
Zawadi hiyo ya picha imekabidhiwa na Mtoto wa
Dkt. Salim Ahmed Salim Bw. Ahmed Salim katika
ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Bw. Ahmed amesema zawadi ya picha iliyotolewa
na Serikali ya China inaonesha picha za Dkt. Salim katika vikao vya Umoja wa
Mataifa, alama na nembo za Serikali ya China ambazo zinaonesha heshima ya nchi hiyo
kwa Dkt. Salim.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.