Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. BaloziLiberata Mulamula amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Anniken Huifeldt katika ofisi za Wizara hiyo tarehe 17 Juni 2022 jijini Oslo, Norway.
Mazungumzo ya mawaziri hao yalihusu juu ya kuimarisha
ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili mathalan katika diplomasia, siasa
na uchumi.
Pamoja na hayo masuala mengine yaliyojadiliwa kwenye
mazungmzo hayo ni pamoja na umuhimu wa kufanyika kwa mageuzi ya kiuchumi ili
kuwa na maendeleo jumuishi kwa wananchi wote, uhuru wa kisisasa na uhuru wa
kuongea ili kuruhusu ushirikishwaji kwa makundi yote katika jamii hususan
wanawake na vijana.
Aidha, nchi za Tanzania na Norway zitaendelea kushirikiana katika
masuala ya afya ili kupunguza vifo vya uzazi, vifo vya watoto na masuala
mengine ya ugonjwa wa UVIKO-19.
Kadhalika viongozi hao wamejadili umuhimu wa usalama na amani katika kusaidia jamii kuinuka kiuchumi na utulivu wa kufanya shughuli za kijamii kwa maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla.
Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Seif Kamtunda wakifuatilia mazungumzo. |
Kutoka kulia Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme, Afisa Ubalozi Norway, Bi. Tunsume Mwangolombe na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Kisa Doris Mwaseba wakifuatilia mazungumzo. |
Wakibadilishana zawadi. |
Picha ya pamoja Mhe. Waziri Mulamula (kati), Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake nchini Sweden, Mhe. Grace Alfred Olutu (wa tatu kulia), Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Elisabeth Jacobsen (wa tatu kushoto) pamoja na ujumbe ulioambana na Mhe. Waziri kutoka Wizarani. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.