Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) amefanya mazungumzo na
Waziri wa Maendeleo wa Denmark, Mhe. Flemming Møller Mortensen (kushoto) pembezoni mwa
Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic
uliofanyika tarehe 14 Juni 2022 jijini Helsinki, Finland.
Mazungumzo baina ya Mawaziri hao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa
kidiplomasia pamoja na kuendeleza sekta za biashara na uwekezaji, uchumi wa
buluu na uchumi wa kijani.
Pia Waziri Mulamula ameishukuru Denmark kwa kuendelea kuwa mdau wa maendeleo
kabla na baada ya Tanzania kupata uhuru wake mwaka 1961 na kwamba Serikali ya
Tanzania inaendelea kusimamia kwa karibu mipango na miradi yote iliyoanzishwa
kwa ushirikiano na Serikali ya Denmark. | Waziri wa Maendeleo wa Denmark, Mhe. Flemming
Møller Mortensen (wa pili kushoto) akieleza kuhusiana na maeneo ya kimkakati
ambayo Serikali ya Denmark itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuenzi
ushirikiano wa kihistoria ulioanzishwa na waasisi wa mataifa hayo mawili. |
Waziri Mulamula akimkabidhi zawadi, Mhe. Mortensen | Ujumbe wa Tanzania ulioambatana na Mhe. Waziri Mulamula ukifuatilia mazungumzo. |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.