Tuesday, June 21, 2022

SERIKALI YASISITIZA KUZINGATIA SHERIA ZA KIMATAIFA, KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU

Na Waandishi wetu, Dar

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeihakikishia Jumuiya ya Kimataifa nchini kuwa inazingatia na kutekeleza sheria za kimataifa za haki za binadamu huku ikiendelea kulinda uhifadhi wa eneo la Ngorongoro.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) leo Jijini Dar es Salaam alipozungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini kuwaelezea mpango wa Serikali katika kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro.

“Napenda kuchukua nafasi hii kuuhakikishia umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania inazingatia na kutekeleza sheria za kimataifa za haki za binadamu na hakuna nanma itaendesha mipango yake kwa kukiuka sheria za haki za binadamu”, alisema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatekeleza mpango wa kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro nchini kwa wananchi kuridhia kuhama kwa hiari yao na kwamba hakuna aliyeondolewa katika eneo hilo kwa nguvu kama inavyoelezwa.

“Tanzania siku zote italinda watu wake, maliasili zake na mipaka yake kwa kuzingatia sheria za kimataifa,” alisema Balozi Mulamula.

Akizungumza katika kikao hicho maalum kwa ajili ya kuielezea Jumuiya ya Kimataifa iliyopo nchini, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kinachoendelea katika eneo la Ngorongoro kwa wakati huu ni uhamaji wa hiari wa wananchi waliokuwa ndani ya eneo la Ngorongoro na sio kwamba kuna uhamishaji wa nguvu unaofanywa na Serikali.

“Serikali imekuja na mpango wa kulinda eneo la Ngorongoro, imechukua miaka 20 kuandaa na kuratibu mpango huu, ambao unatekelezwa sasa na hakuna uhamishaji wa nguvu unaofanywa kwa wanachi kama inavyodaiwa, wananchi husika wameshirikishwa vya kutosha na ndio maana wamekubali na kuamua kuhama kwa hiari wenyewe,” alisema Dkt. Ndumbaro.

Amesema Katiba ya Tanzania inasema watu wote ni sawa na kila mtu ana haki ya kuishi popote na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kulinda na kuheshimu wananchi wake wote bila ya kujali rangi, kabila au dini zao.

Amesema wananchi wamepewa umiliki kwa miaka kadhaa na endapo itaonekana kuna haja ya kuichaukua ardhi hiyo anayeimiliki hulipwa fidia na kupewa ardhi katika eneo lingine na kuongeza kuwa wananchi wanaohama kwa hiari yao kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro wanalipwa fidia na kupatiwa nyumba za makazi, maeneo yenye huduma za kijamii na ardhi kwa ajili ya malisho ya mifugo. 

Naye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema kwamba katika wilaya ya Ngorongoro kuna maeneo mawili ambayo yamekuwa yakizua mjadala ambayo ni eneo la hifadhi la Ngorongoro ambalo ni urithi wa dunia na Pori Tengefu la Loliondo.

Amesema Serikali imechukua uamuzi wa kutekeleza mpango huo kutokana na changamoto kadhaa ambazo zinatishia uhifadhi wa eneo la Ngorongoro na kuongeza kuwa uhamaji wa hiari unaofanyika katika eneo la Ngorongoro una lengo la kuendelea kuhifadhi eneo hilo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.

Akizunguma katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela amewahahakikishia wanadiplomasia nchini kuwa zoezi hilo lilihusisha wananchi wa jumuiya zote waliokuwa wakiishi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kuahidi kuwa majadiliano bado yanaendelea ili kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na uelewa wa pamoja katika suala hilo na hivyo kufanikisha utekelezaji wa azma ya uhifadhi wa hifadhi ya Ngorongoro.

Mkutano huo uliohusisha viongozi waandamizi wa Serikali kutoka Wizara za mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Maliasili na Utalii, Katiba na Sheria pamoja na Wakuu wa Mikoa ya Arusha na Tanga.

Mkutano huo ulilenga kuwafahamisha wanadiplomasia walioko nchini juu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kuhama kwa hiari kunakofanywa na wananchi waliokuwa na makazi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro na hivyo kuondoa sintofahamu iliyokuwepo kuwa wananchi hao wanahamishwa kwa nguvu na serikali na hivyo kukiuka haki za binadamu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini (hawapo pichani) kuwaelezea mpango wa Serikali katika kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini kuwaelezea mpango wa Serikali katika kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza katika kikao na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini (hawapo pichani) kuwaelezea mpango wa Serikali katika kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja akizungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini (hawapo pichani) kuwaelezea mpango wa Serikali katika kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akimkaribisha Waziri wa mambo ya Nje kuzungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini (hawapo pichani) kuwaelezea mpango wa Serikali katika kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro

Balozi wa Visiwa vya Comoro Nchini, Dkt. Ahmada El Badaoui Mohammed  akitoa salamu za shukrani baada ya kikao kati ya Serikali na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini (hawapo pichani)

Mkurugenzi wa Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akiwakaribisha Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa katika mkutano

Mkurugenzi wa Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana akifuatilia mkutano kati ya Serikali na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa

Balozi wa Ufaransa Nchini,  Mhe. Nabil Hajlaoui akichangia katika kikao kati ya Serikali na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini (hawapo pichani) kuwaelezea mpango wa Serikali katika kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro

Baadhi ya Mabalozi katika picha ya pamoja na meza kuu baada ya kikao kati ya Serikali na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini 



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.