Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amesisitiza umoja na mshikamano kwa nchi za Afrika na Nordic aliposhiriki Mkutano wa 19 wa
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nchi za Nordic uliofanyika tarehe
14 Juni 2022 jijini Helsinki, Finland.
Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Mambo
ya Nje wa Finland, Mhe. Pekka Haavisto ambapo aliwakaribisha wajumbe wa mkutano
huo kushiriki mjadala wa vijana wa Nordic – Afrika pamoja na ajenda nyingine za
majadilianao baina ya mawaziri hao.
Akichangia mjadala wa vijana Mhe. Waziri
Mulamula amewasihi vijana waliopata nafasi ya kushiriki katika masuala
mbalimbali ya kimataifa kujitoa kwa dhati ili kuleta tija katika nchi zao
pamoja na kusaidia vijana wengine kupata nafasi hizo.
Sambamba na hilo katika nafasi nyingine ya majadiliano
ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika na Nordic amesisitiza juu ya
umoja na umuhimu wa kushirikiana katika
kukabiliana na changamoto za ulimwengu
kwa manufaa ya wote.
Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa
Nchi za Afrika na Nchi za Nordic pamoja na mambo mengine umejadili masuala ya
amani na usalama, migogoro, mabadiliko ya Tabianchi, masuala ya kimataifa,
vijana na wanawake.
Mkutano wa 19 wa Mamwaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi
za Afrika na Nordic umependekeza Algeria kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 20 wa
Mawaziri hao unaotarajiwa kufanyika mwaka 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Pekka Haavisto ( kulia) akiongoza Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Finland uliofanyika tarehe 14 Juni 2022 jijini Helsinki, Finland. |
Mkutano ukiendelea. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.