Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe, Amina Mohammed jijini Kigali, Rwanda wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola. Mazungumzo hayo yaliangazia masuala makuu matatu ambayo ni mikutano inayoandaliwa na Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Usalama wa Chakula na namna dunia itakavyojikwamua kiuchumi baada ya UVIKO-19.
| Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe, Amina Mohammed wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo.yao yaliyofanyika jijini Kigali, Rwanda. |
| Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Robert Kahendaguza akiwa katika mazungumzo ya utangulizi na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe, Amina Mohammed (mwenye kilemba). Mwingine katika picha ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga.
|
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.