Serikali ya Tanzania na Norway zimeahidi kuanzisha ushirikiano katika masuala ya Bunge kufuatia ziara ya kikazi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Bunge hilo tarehe 17 Juni 2022 jijini Oslo, Norway.
Kufuatia ziara hiyo Mhe. Balozi Mulamula na ujumbe wake walipata
fursa ya kukutana na Wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ulinzi wa Bunge la Norway.
Mhe. Mulamula na Wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ulinzi
walijadili kuhusu umuhimu wa ushirika kwa vyama vya siasa na madhara ya chuki
na uhasama, umuhimu wa kupigania na kujenga amani na umuhimu wa maridhiano kwa
vyama kunapotokea tofauti.
Masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na ulinzi na usalama
katika ukanda wa Afrika na Ukanda wa Ulaya pamoja na madhara mbalimbali
yanayosababishwa na migogoro inayoendelea duniani.
Hata hivyo, Waziri Mulamula ametumia wasaha huo kujadili na
kamati hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazoendelea ulimwenguni na madhara
yake kwa nchi na jamii kwa ujumla. Ameiomba Norway kuendele kufadhili Mfuko wa
Afya, na kushukuru kwa michango mbalimbali kutoka katika hiyo mathalan msaada
wa mapambano juu ya homa ya UVIKO-19.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi wa Bunge la Norway wakijadili juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Bunge la Norwaya na Bunge la Tanzania. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Mhe. Waziri Mulamula na Ujumbe wake wakifuatilia mazungumzo. |
Mazungumzo yakiendelea. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.