Tuesday, March 19, 2013

Katibu Mkuu na Balozi wa India hapa nchini wasaini Mkataba wa Makubaliano kati ya CFR na ICWA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (kulia) kwa pamoja na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Debnath Shaw wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati ya Chuo cha Diplomasia (CFR) cha Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya India (ICWA). Uwekaji saini huo ulifanyika Wizarani leo tarehe 19 Machi, 2013.

Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Mohammed Maundi (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairukiwakishuhudia uwekaji saini wa mkataba huo.

Wajumbe wengine waliohudhuria katika tukio hilo la uwekaji saini wa mkataba. Kutoka kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi wa India hapa nchini, Bw. Gobal Krisha  na Bw. Ali Ubwa, Afisa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha Sheria.

Bw. Haule akibadilishana Mkataba na Balozi Shaw mara baada ya kusaini.


Katibu Mkuu, Bw. Haule pamoja na Balozi Shaw wakionesha Mkataba huo.

Katibu Mkuu Bw. Haule akizungumza na Balozi Shaw mara baada ya kukamilisha zoezi la uwekaji saini mkataba wa Ushirikiano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya India.

Mhe. Balozi Shaw akichangia hoja wakati wa mazungumzo na Bw. Haule huku wajumbe wengine wakisikiliza.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.