Friday, March 15, 2013

Rais Kikwete atuma Salamu za Pongezi kwa Papa Francis I



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Ijumaa 15 Machi, 2013 mchana amemtumia salamu za Pongezi Baba Mtakatifu Francis I kwa kuchaguliwa kwake kuwa Papa wa kanisa Katoliki Duniani na Vatican.

“Kuchaguliwa kwako ni ushuhuda tosha wa imani na heshima kubwa ambayo kanisa Katoliki inayo kwako, historia yako  na upendo wako wa kujali na kuwapenda wanyonge, unyenyekevu ni sababu tosha ya kuwapa wakatoliki, wasio wakatoliki na wasio wakristo pia kusherehekea uteuzi wako” Rais Kikwete amesema kwenye barua yake ya Pongezi kwa Papa Francis I.

Vatican na Tanzania imekua na uhusiano wa muda mrefu na hivyo Rais Kikwete amemhakikishia Papa Francis kuwa uhusiano huo utadumu na anatarajia utaimarika zaidi chini ya uongozi mpya wa Papa Francis I.


“Mwisho”


Imetolewa na:

Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,

IKULU

DAR ES SALAAM

15 March, 2013


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.