Tuesday, March 26, 2013

Ziara ya Rais wa China hapa nchini yamalizika


Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping akiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa pamoja na wake zao Mama Peng Liyuan na Mama Salma Kikwete wakifurahia moja ya kikundi cha burudani kutoka Zanzibar kilichokuwepo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumuaga Mhe. Xi Jinping na Ujumbe wake walipokuwa wanaondoka nchini baada ya kumaliza zaiara yake ya siku mbili
Mhe. Rais Xi Jinping na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete walipokuwa wakisikiliza nyimbo za mataifa yao zikipigwa ikiwa ni ishara ya kumuaga Mhe. Rais Xi Jinping alipomaliza ziara yake ya siku mbili nchini kuanzia tarehe 24 hadi 25 Machi, 2013

Gwaride la Heshima wakati wa sherehe hizo za kumuaga Mhe. Xi Jinping, Rais wa China


Baadi ya Viongozi wa Juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa uwanjani hapo wakati wa sherehe za kumuaga Mhe. Xi Jinping, Rais wa China alipomaliza zaiara yake hapa nchini. Kutoka kulia ni Mhe. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais, Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu, Generali Davis Mwamunyange, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Inspekta Generali wa Polisi, Said Mwema  na Mhe. Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said Mecky Sadick (katikati) na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage wakati wa sherehe za kumuaga Rais wa China, Mhe. Xi Jinping
Rais wa China, Mhe. Xi Jinping akifuatana na mkewe Mama Peng Liyuan wakipanda ndege baada ya kukamilisha ziara yao ya siku mbili hapa nchini

Rais wa China, Mhe. Xi Jinping na mkewe Mama Peng Liyuan wakiwapungia mkono Mhe. Rais Kikwete na ujumbe wake (hawapo pichani)  ikiwa ni ishara ya kuwaaga kabla ya kuingia kwenye ndege tayari kwa kuondoka nchini baada ya kumaliza ziara yao ya siku mbili.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.