Thursday, March 14, 2013

Mhe. Membe akutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akiwa katika mazungumzo na Prof. Harald Braun, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani alipomtembelea Wizarani na kuzungumzia masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani.
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na Prof. Braun huku wajumbe waliofuatana na Katibu Mkuu huyo wa Ujerumani akiwemo Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Mhe. Claus Peter Brandes (mwenye tai nyekundu kushoto)  na wajumbe kutoka Wizarani akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Dora Msechu (wa kwanza kushoto kwa Waziri) wakisikiliza.

Mhe. Membe akifurahia jambo kwa pamoja na Prof. Braun na  Balozi Brandes mara baada ya mazungumzo yao.

Mhe. Membe akiagana na Prof. Braun.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.