Mhe. Thorning-Schmidt pamoja na wenyeji wake wakifurahia burudani kutoka moja ya kikundi cha ngoma ya Kimasaai iliyokuwepo Uwanjani hapo wakati wa mapokezi. |
Mhe. Thorning-Schmidt akilakiwa kwa shangwe na baadhi ya kina mama wa Mkoa wa Arusha |
Mhe. Waziri Mkuu wa Denmark kwa pamoja na Mhe. Waziri Nagu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakipata picha ya pamoja na kikundi cha ngoma wakati wa mapokezi yake Arusha |
Mhe. Thorning-Schmidt akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyopo Jijini Arusha |
Rais wa Mahakama ya ICTR, Mhe. Jaji Vagn Joensen akitoa taarifa fupi ya utendaji wa Mahakama hiyo kwa Mhe. Thorning-Schmidt (hayupo pichani) |
Mhe. Thorning-Schmidt akizungumza na uongozi wa Mahakama ya ICTR (hawapo pichani) mara baada kupokea taarifa kuhusu utendaji wa mahakama hiyo. |
Mhe. Waziri Mkuu, Thorning-Schmidt akivalishwa Vazi Rasmi linalovaliwa na kina mama wa Kimasai mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Wamaasai cha Lepurko kilichopo Wilayani Monduli. |
Mhe. Waziri Mkuu, Thorning-Schmidt akisaini kitabu cha wageni alipowasili kijijini Lepurko |
Mmoja wa kina mama katika Kijiji cha Lepurko akimweleza Mhe. Thorning-Schmidt matatizo yanayowakabili wanawake wa kikiji hicho ikiwa ni pamoja na uhaba wa maji na elimu bora kwa watoto wao. |
Moja ya nyumba maarufu kama "Boma" zilizopo kijijini hapo |
Mhe. Thorning-Schmidt akimsikiliza mmoja wa watoto wa kike ambaye ni mwanafunzi katika kijiji hicho |
Mhe. Thorning-Schmidt akihutubia wananchi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Lepurko |
Mhe. Thorning-Schmidt akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwa shanga na kina mama wa kijijini hapo |
Mmoja wa kina mama wa Kijiji cha Lepurko akimvisha ushanga Mhe. Thorning-Schmidt |
Mhe, Thorning-Schmidt akitoka ndani ya nyumba "Boma" aliyoitembelea kijijini hapo. |
Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika kijiji cha Lepurko. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.