Rais Mteule wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta (kulia) akiwa pamoja na Mhe. William Ruto wakishangilia ushindi.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Kikwete amtumia salamu za pongezi Rais Mteule wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru
Kenyatta
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pongezi nyingi
Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.
Katika
salamu hizo zilizotumwa leo, Jumamosi, Machi 9, 2013, saa chache baada ya
kuthibitishwa rasmi kuwa Mheshimiwa Kenyatta ameshinda Uchaguzi Mkuu wa Kenya
uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii Jumatatu, Machi 4, 2013, Rais Kikwete
amemwambia Mheshimiwa Uhuru Kenyatta:
“Mpendwa
Rais Mteule na Kaka, ilikuwa ni furaha kubwa kwangu kupokea taarifa ya ushindi
wako wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Niruhusu, kwa niaba ya
Serikali na Wananchi wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu binafsi
kukupogenza kwa dhati ya moyo wangu kwa mafanikio haya makubwa ya kuchaguliwa
kwako.”
Ameongeza
Rais Kikwete: “ Ushindi huu ni ushahidi na ishara ya wazi kabisa ya imani na
matumaini ambayo wananchi wa Kenya waliyonayo katika uongozi wako. Huu ni
utambuzi wa kazi yako maridadi na mchango wako mkubwa ambao umeutoa katika
nafasi mbali mbali za uongozi katika siku za nyuma katika jitihada zako za
kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ustawi wa nchi yako na wananchi
wake.”
Amesisitiza
Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua madaraka ya juu zaidi katika nchi yako, napenda
kukuhakikishia msimamo wangu binafsi pamoja na ule wa Serikali yangu wa
kuunga mkono Serikali yako. Ni imani yangu kubwa kwamba pamoja tutaweza
kuendelea kusukuma mbele zaidi maendeleo ya nchi zetu – Kenya na Tanzania na
pia utengamano wa Afrika Mashariki kwa manufaa ya nchi zetu na wananchi wake.”
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
9
Machi, 2013
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.