Tuesday, March 19, 2013

Mhe.Naibu Waziri akutana kwa mazungumzo na Katibu Mtendajii wa Kamisheni ya Uchumi ya UN kwa Afrika

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Bara la Afrika, Bw. Carlos Lopes,  Ofisini kwake leo tarehe 19 Machi, 2013 ambapo walizungumzia masuala mbalimbali ya ukuzaji uchumi hapa nchini ikiwemo maendeleo ya viwanda.

Mhe. Maalim akiwa katika mazungumzo na Bw. Lopes.

Mhe. Maalim akimsikiliza kwa makini Bw. Lopes wakati wa mazungumzo yao.

Mhe. Maaalim akifafanua jambo kwa Bw. Lopes wakati wa mazungumzo yao. Mwingine katika picha ni Bw. Antonio Pedro, Mkurugenzi wa Kamisheni hiyo kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mhe. Maalim akimweleza jambo Bw. Lopes (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Bw. Nathaniel Kaaya (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Ali Mwadini (mwenye tai nyekundu), Msaidizi wa Naibu Waziri na Bw. Macocha Tembele (kulia), Afisa Mambo ya Nje katika Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa.


Mhe. Maalim na wajumbe wengine wakimsikiliza Bw. Lopes.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.