Tuesday, March 26, 2013

Rais Kikwete na Rais Xi Jinping walipotembelea Makaburi ya Wataalam wa China huko Majohe

Mashada ya Maua yakiwa yamewekwa kwenye moja ya kaburi la Wataalam kutoka China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA. Makaburi hayo zaidi ya 60 yapo katika eneo la Majohe-Ukonga nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China wakitoa heshima zao kwenye makaburi hayo.


Sehemu ya Gwaride Maalum lililoandaliwa wakati wa utoaji heshima kwa Wataalam hao wa China waliozikwa katika eneo hilo.

Mhe. Rais Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kuwakumbuka Wataalam hao huku Mhe. Rais Xi pamoja na Mke wake, Mama Peng Liyuan na Mama Salma Kikwete wakishuhudia.

Mhe. Rais Xi Jinping naye akisaini kitabu hicho cha kumbukumbu.

Mhe. Rais Kikwete akitoa hotuba fupi kuwakumbuka wataalam hao ambao aliwaelezea kama mashujaa.

Mhe. Rais Xi Jinping naye aliungana na Mhe. Rais Kikwete kuwakumbuka Wataalam hao ambao aliwaelezea kama marafiki wa kweli kwa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.