Mhe. Thorning-Schmidt akizungumza na mmoja wa kina mama waliolazwa hospitalini hapo kuhusu maendeleo ya afya ya mtoto wake. |
Mhe. Thorning-Schmidt akiwa amembeba mtoto mmoja alipotemebelea Wadi ya Watoto katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu |
Mhe. Thorning-Schmidt akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Afya kilichopo katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu. |
Wanafunzi wa Chuo hicho wakimsikiliza Mhe. Thorning-Schmidt (hayupo pichani) alipozungumza nao. |
Mhe. Thorning-Schmidt akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbulu. |
Baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbulu wakimsikiliza Mhe. Thorning-Schmidt alipozungumza nao |
Mhe. Thorning-Schmidt akisalimiana na Dkt. Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mara baadaya kuwasili Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha. |
Picha ya Pamoja kati ya Mhe. Thorning-Schmidt, Mhe. Waziri Nagu, Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na baadhi ya wajumbe aliofuatana nao katika ziara yake. |
Mhe. Thorning-Schmidt akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha TCDC kilichopo Usa River mkoani Arusha. Kituo hicho kinafadhiliwa na Denmark na kilianzishwa miaka 40 iliyopita. |
Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na Mhe. Waziri Nagu mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Arusha. |
Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Magesa Mulongo mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani humo. |
Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na viongozi mbalimbali waliofika kumsindikiza. |
Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na Balozi wa Denmark hapa nchini Mhe. Johnny Flento mara baada ya kuhitimisha ziara yake. |
Mhe. Thorning-Schmidt akielekea kupanda ndege tayari kwa kuondoka nchini. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.