Friday, March 22, 2013

Mhe. Membe azungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Rais wa China hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo tarehe 22 Machi, 2013 kuhusu ziara ya kitaifa ya siku mbili ya Rais mpya wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping atakayoifanya hapa nchini kuanzia tarehe 24 hadi 25 Machi, 2013. Wengine katika picha ni Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Wizara  wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Baadhi ya Waandishi kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari vya hapa nchini wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao kuhusu ziara ya Rais wa China, Mhe. Xi Jinping hapa nchini.

Kundi jingine la Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini taarifa ya Mhe. Membe kuhusu ziara ya Rais wa China hapa nchini.


Waandishi kutoka mashirika mbalimbali ya habari ya China pia walikuwepo kwenye mkutano huo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha (kulia) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Philip Marmo (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Bertha Semu-Somi wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais wa China hapa nchini

Mmoja wa waandishi wa habari kutoka China akiuliza swali kwa Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mkutano kuhusu ziara ya Rais wa China hapa nchini

Mhe. Membe, Mhe. Maalim, Bw. Haule na Balozi Gamaha wakisikiliza swali kutoka kwa Mwandishi wa Habari (hayupo pichani) wakati wa mkutano kuhusu ziara ya Rais wa China, Mhe. Xi Jinping hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.