Thursday, March 28, 2013

Mhe. Rais apokea Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa UAE hapa nchini



Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Abdulla Ibrahim Al-Sowaidi, Balozi mpya wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) hapa nchini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 28 Machi, 2013.


Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisalimiana na  Balozi Mpya wa UAE hapa nchini Mhe.  Al-Sowaidi mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete.

Mhe. Al-Sowaidi, Balozi Mpya wa UAE hapa nchini akisalimiana na  Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa huku Mhe. Membe na Bw. Hangi Mgaka (kushoto), Afisa Mambo ya Nje wakishuhudia.

Mhe. Al-Sowaidi, Balozi mpya wa UAE hapa nchini akiwa katika mazungumzo na Mhe. Rais Kikwete mara baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho.

Mhe. Membe (kushoto) akiwa na wajumbe wengine wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Rais Kikwete na Balozi mpya wa UAE hapa nchini, Mhe. Al-Sowaidi (hawapo pichani). Kulia ni Balozi Liberata Mulamula, Mshauri Mwandamizi wa Rais wa masuala ya Diplomasia na Balozi Simba Yahaya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Balozi Al-Sowaidi akisaini  Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.



Mhe. Balozi Al-Sowaidi (katikati) akisikiliza Wimbo wa Taifa lake ulipokuwa ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais. Kulia ni Balozi Mohammed Maharage, Mkuu wa Itifaki na Bw. Shaaban Gurumo, Mnikulu.



Wajumbe wengine wakati Mhe. Balozi Al-Sowaidi akipokea heshima mara baada ya kuwasili Ikulu. Kushoto ni Bw. I. Kimario, ADC na Bw. Cosato Chumi, Afisa Mambo ya Nje katika Idara ya Itifaki.

Bendi ya Polisi ikipiga nyimbo za taifa la UAE na Tanzania kwa heshima ya Balozi mpya wa UAE, Mhe. Al-Sowaidi (hayupo pichani) hapa nchini.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.