Friday, May 5, 2017

Wizara ya Mambo ya Nje yapokea magari ya msaada




 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) (katikati), akipokea funguo za Magari aina ya Toyota Land Cruiser  kutoka kwa  Balozi wa Omani hapa nchini, Mhe. Ali Abdullah Al Mahruqi. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam leo. Baada ya kukabidhiwa magari hayo yenye thamani ya takriban milioni 400 za Tanzania, Waziri Mahiga alisema kuwa msaada huo umetolewa na Serikali ya Oman kwa ajili ya kusaidia masuala ya usafiri katika kipindi hiki cha mpito ambapo Serikali inahamia Dodoma. 
Waziri Mahiga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali na Wizara yake kwa ujumla mara baada ya kupokea msaada huo. 
Waziri akiendelea kuongea huku Watumishi wa Wizara yake wakimsikiliza kwa makini.
Balozi Al Mahruqi naye akizungumza na kuishukuru Tanzania kwa ushirikiano anaoumpata kwenye utendaji kazi wake hapa nchini. Alisema Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo huduma za kijamii.
Sehemu ya viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Bw. Mapesi Manyama, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika,  Bw. Suleiman Saleh; Mhasibu Mkuu, Bw. Paul Kabale; Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora, Bi. Tagie Daisy Mwakawago na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga,


Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Martin (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Innocent Shiyo (wa kwanza kulia) wakiwa na sehemu ya Watumishi wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza kwa makini Dkt. Mahiga na Balozi wa Oman
Sehemu ya Madereva wa Wizara nao walihudhuria shughuli hiyo ikiwa wao ndio waendeshaji wa Magari hayo.
Sehemu nyingine ya watumishi na wageni waliohudhuria shughuli hiyo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala akimkabidhi funguo za magari Afisa Usafirishaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Mkenda

Picha ya pamoja mara baada ya shughuli kumalizika.

Waziri Mahiga awa Mgeni rasmi hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Israeli, Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga jana alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Taifa la Israeli yaliyo fanyika mjini Dodoma katika Hoteli ya Morena.

Hafla hiyo ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Taifa hilo na uhusiono mzuri wa kidiplomasia  baina ya Tanzania na Israeli yaliratibiwa na Ubalozi wa Israel wenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Waziri Mahiga akizungumza katika hafla hiyo aliupongeza Ubalozi wa Israel kwa uamuzi wake wa kufanyia hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wao, Makao Mkuu ya Serikali mjini Dodoma. Waziri Mahiga aliongeza kusema Mataifa haya mawili Tanzania na Israel yana mahusiano mazuri ya kidiplomasia, ikidhihirishwa wazi na idadi kubwa ya raia wa nchi hizi mbili kutembeleana na kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo utalii.

Aidha Mahiga aliipongeza Serikali ya Israel kwa hatua kubwa ya maendeleo waliyofikia katika maeneo mbalimbali ikiwemo sayansi na teknolojia na kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali. 

Balozi wa Israeli nchini Mhe. Yahel Vilan mwenye makazi yake Jijini Nairobi, Kenya akitoa hotuba yake alisema Ubalozi wa Israeli umechukua maamuzi ya kufanyia hafla hiyo Mjini Dodoma ikiwa nikuunga mkono maamuzi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Dodoma. Aliongeza kusema kuwa hafla hiyo ni ishara ya Israel kuanziasha Ubalozi wake nchini Tanzania.

Balozi Vilan ameihakikishia serikali ya Tanzania kuwa Israel itaendelea kuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Taifa katika maeneo ya kilimo, afya, elimu, sayansi na teknolojia na usalama.

Israeli ilifungua kituo cha kushughulikia masuala ya viza nchini Tanzania tarehe 3 Novemba, 2016.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 69 ya uhuru wa Taifa la Israel iliyofanyika kwenye Hoteli Morena Mjini Dodoma



Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo ya Taifa unakipigwa kweye maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Israel

Balozi wa Israeli nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya  Mhe. Yahel Vilan akizunguza kwenye hafla ya maadhimisho ya  69 ya uhuru wa Israel iliyofanyika mjini Dodoma

Mhe. Balozi Vilan akisisitiza jambo

Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akihutubia hadhira iliyo shiriki hafla hiyo

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi (kushoto) akifuatilia jambo, kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima

Picha ya pamoja

Picha ya pamoja

Tuesday, May 2, 2017

AMBASSADOR WILFRED JOSEPH NGIRWA HONOURED BY UN FOOD AND AGRICULTURAL ORGANIZATION

AMBASSADOR NGIRWA TOGETHER WITH AMBASSADOR GEORGE K. MADAFA.
AMBASSADOR NGIRWA TOGETHER WITH HIS WIFE.
AMBASSADOR NGIRWA TOGETHER WITH THE DIRECTOR GENERAL DR. GRAZIANO DE SILVA

******************************

Ambassador Wilfred Joseph Ngirwa was honoured by unvailing his portrait in the UN Food and Agricultural Organization in Rome during the Session of the FAO Council which was held from 24- 28 April 2017.

Ambassador Ngirwa, the current Independent Chairperson of the UN Council, was unanimously elected unopposed by Member Nations of the FAO to serve in his capacity in 2013. Previously, he was the Ambassador of Tanzania as Permanent Representative to the UN Food Agencies in Rome, Italy.

The Ambassador of Tanzania in Italy H.E George Kahema Madafa represented Tanzania in the FAO Council
Session and witnessed the unvailing of portrait ceremony of Ambassador Ngirwa.

Watumishi wa Wizara washiriki maadhimisho ya sherehe ya Siku ya Wafanyakazi

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo wameungana na Wafanyakazi wengine Duniani katika maadhidhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika matembezi maalumu ya siku ya Wafanyakazi Duniani

Watumishi wa Wizara wakiwa katika  matembezi ya maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Meo


Saturday, April 29, 2017

Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watoa elimu ya Mtangamano kwa Wanachuo



Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Wabunge wa Watanzania katika Bunge hilo Mhe. Makongoro Nyerere (aliyesimama) akizungumza wakati wa semina ya kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika katika Chuo cha Mipango cha Mjini Dodoma. 
Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akijibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe waliohudhuria semina hiyo.

Meza kuu wakifuatilia semina 
Mbunge Mhe. Makongoro Nyerere (wapili kushoto) akikabidhi machapisho kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango Prof.Hozen Mayaya. wengine ni baadhi ya Bunge wa Bunge walioshiriki semina hiyo


Sehemu ya wanafunzi wa Chuo cha Mipango wakifuatilia semina

Wanafunzi wakifuatilia semina

Picha ya pamoja

Friday, April 28, 2017

Tanzania na Jamhuri ya Korea zaadhimisha miaka 25 ya Ushirikiano wa Kidiplomasia

Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na Korea. Katika hotuba hiyo Tanzania iliishukuru Jamhuri ya Korea kwa kuendelea kuwa marafiki wakubwa wa Tanzania na kushirikiana kwenye kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali zikiwemo kujenga miundombinu muhimu kama barabara na madaraja.
Rais wa Taasisi ya Sera ya Sayansi na Teknolojia ya Jamhuri ya Korea, Dkt. Jong Guk Song  naye akizungumza katika maadhimisho hayo,
Sehemu ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa kwenye maadhimisho hayo
Sehemu nyingine ya wageni kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Korea nchini
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi Mindi Kasiga akitoa ufafanuzi wa ratiba na mpangilio wa matukio wakati wa maadhimisho hayo.
Sehemu ya Watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioshiriki maadhimisho hayo.
Balozi Mteule wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea, Mhe. Matilda Masuka naye alihudhuria maadhimisho hayo
Picha ya pamoja.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Mkurugenzi wa IFAD Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo-IFAD wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bw. Sana Jatta alipofika Wizarani tarehe 28 Aprili, 2017. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya kuendeleza miradi ya kilimo na ufugaji hapa nchini kwa ajili ya kujihakikishia usalama wa chakula na lishe bora kwa maendeleo.
Sehemu ya ujumbe kutoka Ofisi za IFAD hapa nchini alioambatana nao Bw. Jatta. Kulia ni Bw. Francisco Pichon, Mwakilishi na Mkurugenzi wa IFAD nchini akiwa na Bi. Mwatima Juma Afisa Miradi Mwandamizi wa IFAD nchini.
Bw. Jatta nae akimweleza jambo Mhe. Dkt. Susan wakati wa mazungumzo yao.


Sehemu ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Jestas Nyamanga, Bi. Eva Ng'itu, Afisa Mambo ya Nje na Bw. Charles Faini, Msaidizi wa Naibu Waziri.
Mhe. Dkt. Kolimba katika picha ya pamoja na wageni wake.

Thursday, April 27, 2017

Wabunge wa EALA watoa elimu ya fursa za Mtangano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Wafanyabiashara wa Dodoma

Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Adam Kimbisa akizungumza na wajumbe kwenye semina ya kutoa elimu ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kuhamasisha fursa zinazotokana na mtangamano huo kwa wafanyabiasahara wa mjini Dodoma. Semina hiyo inayohusisha wafanyabiashara na makundi mbalimbali katika jamii pamoja na mambo mengine inalenga kuongeza urari wa biashara wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; semina hii itaendelea kesho Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Stephen Mbundi akifafanua jambo kwenye semina hiyo. Bw. Mbundi alitumia fursa hiyo kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali yaliyoulizwa na wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki semina hiyo.

Mmoja wa wajumbe akizungumza katika semina hiyo

Semina ikiendelea

Mmoja wa wajumbe kutoka kundi la wafanyabiashara akizungumza


Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania wanaowakilisha Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (kulia) akikabidhi bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwakilishi wa wafanyabiashara mara baada ya semina