Wednesday, November 20, 2013

Kuwait kuzipatia nchi za Afrika mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya Dola bilioni moja, Amir


 
 
Na Ally Kondo, Kuwait

Serikali ya kuwait imetenga kiasi cha Dola za Marekani bilioni moja (1) kwa ajili ya kuzipatia nchi za Afrika mikopo ya masharti nafuu katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Tangazo hilo lililotolewa na Amir wa Kuwait ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Ushirikiano baina ya Nchi za Afrika na Kiarabu (Third Afro Arab Summit), Sheikh Sabah Al-Ahnad Al-Sabah wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi ya mkutano huo nchini Kuwait siku ya Jumanne tarehe 19 Novemba, 2013.

Sanjari na kiasi hicho cha fedha, Sheikh Al-Sabah alitangaza kiasi kingine cha Dola za Marekani milioni moja (1) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za utafiti zenye lengo la kuibua fursa za maendeleo katika nchi za Afrika.

 
Sheikh Al- Sabah aliwambia wajumbe wa mkutano huo kuwa, Mkutano wa Tatu wa Afro Arab Summit unafanyika huku nchi nyingi za Afrika na Kiarabu zikikabiliwa na changamoto za kisiasa na kiuchumi ambazo bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu malengo yanaayowekwa katika mikutano hiyo hayatafikiwa. Alisisitiza nchi za Afrika na Kiarabu kuwekeza katika miradi itakayoimarisha ushirikiano wao akitolea mfano wa sekta ya kilimo. “Endapo usalama wa chakula hautakuwa wa kuaminika katika nchi za Afrika na Kiarabu, kutazifanya nchi hizo kuwa katika hali tete na hatimaye kushindwa kukidhi matarajio ya wananchi wao. Sheikh Al-Sabah alisikika akisema.

 
Aidha, Amir wa Kuwait aliwaomba Wakuu wa Nchi kutumia mkutano huo kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro unaoendelea nchini Syria ambao athari zake unaikumba kanda nzima ya Kiarabu. Alihitimisha hotuba yake kwa kulitolea wito Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuishinikiza Israel itekeleze Maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mamlaka ya Palestina.

 
Kwa upande wake, Mwenyekiti mwenza wa mkutano huo, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Hailemariam Dessalegn alieleza kuwa nchi za Afrika haziwezi kufikia mapinduzi ya kijani endapo hakutawekwa mkazo katika sekta za nishati jadilifu, miundombinu na utalii. Hivyo, alisisitiza umuhimu wa mkutano huo kubuni mwongozo makini wa ushirikiano utakaowezesha kufikiwa kwa malengo hayo.  

 

Mhe. Dessalegn alizihimiza nchi za Afrika na Kiarabu kuongeza nguvu mara dufu katika mapambano dhidi ya uharifu wa mipakani, ugaidi, uharamia pamoja na uhamaji wa kinyume cha sheria. Aliweka angalizo kuhusu tatizo la uhamaji kwa kusema kuwa endapo halitafanyiwa kazi vizuri linaweza kudhoofisha ushirikiano huo. Hivyo, aliunga mkono pendekezo la kuunda Kamati ya Pamoja ya Wataalamu kutoka nchi za Afrika na Kiarabu ili kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

 

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Nkosazana Dlamini-Zuma naye aliwahakikishia Wakuu wa Nchi katika mkutano huo kuwa, Afrika imejizatiti kutekeleza yale yote mazuri yatakayoafikiwa katika mkutano huo. Aidha, alihimiza umuhimu wa kuwekeza katika elimu ili idadi kubwa ya vijana ambao ndio nguvu kazi na wanawake ambao ni zaidi ya nusu katika nchi za Afrika wapate elimu bora inayoendana na madadiliko yanayotokea duniani hivi sasa.

 

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais ambaye pia amepangiwa kutoa hotuba.

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal wa pili kutoka kushoto akisikiliza ahadi ya Amir wa Kuwait ya kuzikopesha  nchi za Afrika Dola za Marekani biliomni moja.


Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Prof. Abdillah Omar wa kwanza kushoto, Mbunge wa Wawi, Mhe. Ahmadi Rashidi na Mbunge wa Gando, Mhe. Khalifa Khalifa nao walishuhudia ahadi ya Amir wa Kuwait.


Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz mwenye ushungi mwekundu na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Simba Yahya nao walikuwepo katika ukumbi wa mkutano wakati Amir wa Kuwait akitoa hotuba.

Tuesday, November 19, 2013

CHOGM 2013 Final Communique


H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete (see Tanzania national flag in the background) of the United Republic of Tanzania as he enters the Nelum Pokuna Mahinda Rajapaksa Theatre in Colombo City during the opening ceremony of the CHOGM 2013 in Colombo, Sri Lanka.  

Heads of State and Government of Commonwealth in a group photo before issuing a joint Final Communique for the CHOGM 2013. 



Monday, November 18, 2013

Dkt. Bilal kuongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Afro Arab Summit

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Mohamed Gharib Bilal akiongea na ujumbe wake {haupo pichani}wakati wa kikao cha maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa Afro Arab Summit utakaofanyika nchini Kuwait tarehe 19 na 20 Novemba, 2013. kikao hicho kilifanyika katika moja ya kumbi za Jumba la Mfalme wa Kuwait.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe {Mb}, akitoa taarifa kwa Makamu wa Rais kuhusu masuala yatakayojadiliwa katika Mkutano wa Afro Arab Summit.


Mbunge wa Wawi, Mhe. Hamadi Rashidi naye akichangia jambo kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Afro Arab Summit. Aliyevaa kofia ni Mbunge wa Gando, Mhe. Khalifa Khalifa.

Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz akichangia hoja katika kikao hicho.

Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa sita kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake katika mkutano wa Afro Arab Summit.

Mkutano wa Mawaziri wa Afro Arab Summit umefunguliwa

 

Meza Kuu ikionesha baadhi ya Viongozi wa Mkutano wa Mawaziri wa Afro Arab Summit wakiwa wameketi.

Mwenyeki wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Nkosazana Dlamini-Zuma akihutubia Mkutano wa Mawaziri wa Afro Arab Summit.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Mhandisi Christopher Chiza {Mb}akifuatilia kwa makini mkutano wa Mawaziri.

Ujumbe wa Tanzania, kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Gregory Teu {Mb}, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Uledi Mussa, Mhe. Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakati wa mkutano huo.

Tanzania na Kuwait zasaini Mkataba wa Kulinda na Kukuza Vitega Uchumi pamoja na Mkataba wa Kushitrikiana katika Masuala ya Utalii

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe {Mb} aliye kushoto akiongea na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Khalid Al-Sabah kabla ya shughuli ya kusaini Mikataba kuanza.
 




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe {Mb} na Waziri mwenzake wa Kuwait wakisaini Mikataba ya Kukuza na Kulinda Vitega Uchumi; na Kushirikiana katika Masuala ya Utalii. Uwekaji saini huo ulifanyika nchini Kuwait siku ya Jumapili tarehe 17 Novemba, 2013.

Picha zaidi za uwekaji saini huku Maafisa kutoka Wizara za Mambo ya Nje za Tanzania na Kuwait wakishuhudia. kushoto ni Bw. Benedict Msuya kutoka Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe {Mb} na mwenzake wa Kuwait wakipongezana baada ya kukamilisha kazi ya kuweka saini Mikataba, Wanaopiga makofi ya furaha kutoka kushoto ni Mhe. Prof. Abdillah Omar, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia ambaye anawakilisha pia Kuwait na Qatar na anayefuata ni Mhe. Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Waheshimiwa Mawaziri wakibadilishana Mikataba mara baada ya kuisaini huku Balozi Yahya akipiga makofi kwa furaha.

Waheshimiwa Mawaziri wakiteta jambo baada ya kukamilisha kazi ya kusaini Mikataba.

Mhe. Membe akiongea na ujumbe wake, Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Clifford Tandari , Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Fedha, Bw. Charles Samanyi, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia ambaye pia anashughulikia masuala ya Afro Arab, Mhe. Naimi Aziz na Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje. 

Sunday, November 17, 2013

Naibu Waziri atunukiwa Shahada ya Uzamivu

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akitafakari wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo Mhe. Dkt. Maalim alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika masuala ya Sheria.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Balozi Nicholaus Kuhanga akimtunuku Shahada ya Uzamivu (Ph.D) Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) katika Mahafali ya 43 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani tarehe 16 Novemba, 2013. Mhe. Dkt. Maalim alikuwa miongoni mwa Wahitimu 41 waliotunukiwa Shahada ya Uzamivu siku hiyo.

Mhe. Dkt. Maalim na Wahitimu wengine wa Shahada ya Uzamivu wakiwa wenye nyuso za furaha.

Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, Mhe. Balozi Fulgence Kazaura (katikati mwenye joho jekundu) akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Rwekaza Mukandala (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Wahadhiri wengine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo hicho.

Wahitimu wa Shahada na Stashahada mbalimbali.

Picha ya pamoja



Mhe. Dkt. Maalim (katikati) akiwa na Wahitimu wenzake. Kushoto ni Dkt. Adelardus Kilangi na Dkt. Mramba Joseph (kulia)

Mhe. Dkt. Maalim akiwa na Wahitimu wengine wakiimba Wimbo wa Taifa.

Mhe. Dkt. Maalim akiwa na Mke wake mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu.

Mhe. Dkt. Maalim na Familia yake.

Foreign Minister Bernard Membe elected Chair of CMAG


Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operatin humbly accepting his appointment as a new Chairperson for the Commonwealth Ministerial Action Group (CMAG), a meeting that was held today at the Bandaranaike Memorial International Conference Hall (BMICH) in Colombo, Sri Lanka. 

The Commonwealth Ministerial Action Group in session during their meeting today held at the Bandaranaike Memorial International Conference Hall (BMICH) in Colombo, Sri Lanka. 

Minister Membe (2nd left) and Hon. Prof. G.L. Peiris, Sri Lankan External Affairs Minister reviewing Presidential election report on Maldives from the Commonwealth team of observers. 

Hon. Minister Membe (right), congratulates his counterpart Sri Lankan External Affairs Minister Hon. Prof. G.L. Peiris (left),for his country as a host of the Commonwealth Heads of Government Meeting (CHOGM) and for the heartfelt hospitality throughout the weeklong meetings. 

The Sri Lankan External Affairs Minister  Hon. Prof. G.L. Peiris congratulates Hon. Minister Bernard Membe for been elected as a new CMAG Chairperson. 

Mr. Kamalesh Sharma (left), Commonwealth Secretary-General congratulates Hon. Minister Membe. 

Hon. Samura M. W. Kamara, Sierra Leone Minister for Foreign Affairs and International Cooperation congratulates Hon. Minister Membe. 

Minister Membe (right), in a discussion with Ms. Mmasekgoa Masire-Mwamba (center), the Commonwealth Deputy Secretary-General and Ambassador Peter Kallaghe (left), High Commissioner of the United Republic of Tanzania in London, with accreditation to the United Kingdom, to the Republic of Ireland and to the Commonwealth.

Hon. Minister Membe gets congratulations from representative of the Cyprus Foreign Affairs Minister (left) and from the representative of the New Zealand Foreign Affairs Minister.

Hon. Minister Membe, who is a new CMAG Chairperson, in a photo with Ms. Mmasekgoa Masire-Mwamba (left), the Commonwealth Deputy Secretary-General and a representative of the Guyana Foreign Affairs Minister (right)

Hon. Minister Membe (2nd right), in a group photo with Ambassador Kallaghe (2nd left), together with Foreign Service Officers Mr. Amos Msanjila (left) and Ms. Eva Ng'itu (right), from the Tanzania Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 

Hon. Minister Membe (center), in a photo with Ambassador Kallaghe (left) and Ambassador Celestine Mushy, Director of the Department of Multilateral Co-operation in the Tanzania Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.

Foreign Service Officer Ms. Eva Ng'itu congratulates Hon. Minister Membe. 

Foreign Service Officer Mr. Amos Msanjila congratulates Hon. Minister Membe. 

Communication Officer Ms. Tagie Daisy Mwakawago congratulates hon. Minister Membe for his appointment as a new CMAG Chairperson.

Hon. Minister Membe (left), held discussion with Ambassador Kallaghe (2nd left)Prof. Severine Rugumamu (2nd right) and Ambassador John William Herbert Kijazi (right) High Commissioner of the United Republic of Tanzania in India with accreditation to the Democratic Socialist Republic of Sri Lanka.  Minister Bernard K. Membe (MP) was unanimously elected Chairperson of the Commonwealth Ministerial Action Group on the Harare Principles (CMAG) in Colombo, Sri Lanka today.

Congratulations to Ms. Eva Ng'itu and Mr. Amos Msanjila for a job well done!


Foreign Minister Bernard Membe elected Chair of CMAG

By TAGIE DAISY MWAKAWAGO

Colombo, Sri Lanka

Tanzania Foreign Minister Bernard K. Membe (MP) was unanimously elected Chairperson of the Commonwealth Ministerial Action Group on the Harare Principles (CMAG) in Colombo, Sri Lanka today.

“We appoint you as our new Chairperson because of your strong institutional knowledge and active mind,” said Hon. Samura M. W. Kamara, Sierra Leone Minister for Foreign Affairs and International Cooperation.  He said that the decision to elect Tanzania was easy, hoping that Tanzania will continue to spearhead CMAG’s values during the tenure. 

The eight group members of CMAG comprised of Commonwealth countries of Cyprus, India, Sri Lanka, Solomon Islands, Pakistan, Guyana, New Zealand and Sierra Leone expressed their confidence with Tanzania Foreign Minister Membe for his experience and wisdom.  Tanzania sums up the total nine group members of CMAG.

The Commonwealth Ministerial Action Group also elected Hon. Murray McCully, Foreign Minister of New Zealand as a Vice-Chair.

Speaking as a new CMAG Chair, Hon. Membe said that he appreciated tremendously the unanimous support received from fellow members.  “I am truly humbled by your decision to elect me as your new Chair.  I assure you of my unwavering commitment in protecting the core groundwork that CMAG stands for,” said Minister Membe.

The Ministers also jointly agreed the removal of Maldives from CMAG’s formal agenda, after receiving an update from the Commonwealth observers that the Presidential elections held this week in that country were declared credible and peaceful. Earlier this week CMAG had agreed to table Maldives on the Group’s formal agenda pending free and fair presidential elections in the country.

In a joint statement issued after their meeting, the Ministers congratulated the people of Maldives for showing their firm commitment to democracy, and for exercising their franchise in record numbers.  “We welcomed the successful conclusion of the presidential election and noted the interim statement of the Commonwealth Observer Group, which stated that the election had been ‘credible and peaceful’, noted the CMAG statement. 

Commenting on Sri Lanka as host of the Commonwealth Heads of Government Meeting, Minister Membe congratulated the country for their hospitality and commitment in restoring normalcy.  “You have demonstrated good leadership and endurance despite the turbulences you had faced in the past,” said Minister Membe.

On his part, Sri Lankan External Affairs Minister Prof. G.L. Peiris said that hosting CHOGM had enabled foreign representatives to witness his country emerging from the shadow of war conflicts.  “This is a true characteristic of our Sri Lankans for their resilience and ability to bounce back,” said Prof. Peiris.

Minister Membe has been in Sri Lanka for the past three days participating in the Foreign Ministers side-meetings as a preparatory meeting of the Commonwealth Heads of Government Meetings (CHOGM).  President Kikwete led the Tanzania delegation and participated in the Heads of State meetings from 15-17 November here in Sri Lanka.   


End.




Saturday, November 16, 2013

Tanzania yang`ara eneo bora kiuwekezaji

Mhe. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara akizungumza kwenye jukwaa la masuala ya biashara la Nchi Wanachama wa  Jumuiya ya Madola  (CBF), jana nchini Sri Lanka.


Tanzania yang`ara eneo bora kiuwekezaji



Tanzania inang’ara na kupanda chati kama eneo bora kiuwekezaji,  kufuatia kujijengea heshima iliyoletwa  na ziara ya Rais wa China Xi Jinping na Barack Obama wa Marekani,  ambao ni viongozi wanaoheshimika kote  duniani .

Haya yalisemwa nchini Sri Lanka kwenye jukwaa la masuala ya biashara la Nchi Wanachama wa  Jumuiya ya Madola  (CBF). Jumuiya hiyo inaundwa na yaliyokuwa makoloni ya Uingereza.

Kadhalika jukwaa hilo lilithibitishiwa kuwa imekuwa rahisi kwa  Tanzania kutambulika kama taifa shindani kiuwekezaji linaloweza kuchuana na majirani zake na mataifa mengine  ya Afrika.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda,  alitoa maelezo hayo wakati akizungumza na wajumbe wa jukwaa hilo na kuongeza kuwa faida iliyopatikana kwenye  miradi ya uwekezaji inayoendeshwa na kampuni za ndani na za kigeni imebakizwa nchini kwa ajili  ya kuendeleza uzalishaji.

Hata hivyo, si Waziri Kigoda wala Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar Mwinyikai, alitaja kiasi cha faida hiyo iliyopatikana na kubakizwa nchini kwa ajili ya uwekezaji zaidi.

Aliwaambia wajumbe kuwa serikali inatekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa  pia inajizatiti kuimarisha maeneo ya taasisi za fedha, teknolojia ya habari na mawasiliano  na maboresho ya kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC)  kukifanya kuwa na uwezo kwa kutoa huduma na mahitaji yote ya wawekezaji.

Sri Lanka pamoja na Tanzania zinaangalia uwezekano wa kuwa na ushirikiano kwenye kuboresha miundombinu na uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam.

Hatua hiyo inakuja wakati Sri Lanka inajenga bandari ya kisasa iitwayo ‘Colombo port city’ ambayo baadhi ya wadau wanaikosoa kuwa itakuwa tishio kwa bandari nyingi ikiwamo   Singapore ambayo ni bandari  huru na kubwa duniani iliyoko kwenye bahari ya Hindi, ikiunganisha mataifa ya Mashariki na Magharibi .

Akizungumza kwenye jukwaa hilo  Mkurugenzi Mtendaji wa TIC  Juliet Kairuki, alisema Tanzania ina uwezekano mkubwa wa kupata wawekezaji zaidi baada ya kuthibitika kuwa ni taifa lisilo na migogoro ya kisiasa.

Alitoa mfano kuwa TIC imepokea maombi ya uwekezaji kwenye nishati ya  joto la asili la ardhini (geothermal) kutoka kampuni ya Marekani wenye thamani ya Dola  milioni 28 (sawa na Sh. bilioni 45.5).


Source:  The Guardian