Wednesday, July 3, 2013

Matukio mbalimbali yaliyofanyika wakati wa Mkutano wa Wake wa Marais wa Afrika



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi Mkutano wa Wake wa Marais wa Afrika uliofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 2 na 3 Julai 2013. Mkutano huo unafadhiliwa na Taasisi ya George W. Bush, Jr.

Mke wa Rais, Mhe. Mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya kuwakaribisha nchini Wake za Marais kutoka nchi za Afrika katika mkutano wao uliofanyika Jijini Dar es Salaam  tarehe  2 na 3 Julai, 2013. Pamoja na mambo mengine mkutano huo ulijadili masuala mbalimbali yanayoweza kuwainua wanawake Barani Afrika ikiwa ni pamoja na Elimu. Ujasiriamali na Afya Bora.

Mke wa Rais wa zamani wa Marekani, Mama Laura George W. Bush, Jr. akitoa neno la shukrani kama mfadhili wa mkutano huo.


Baadhi ya Wake wa Marais wakisikiliza hotuba ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani).

Wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wa Wake wa Marais
Mke wa Rais wa Marekani, Mhe. Mama Michelle Obama akichangia hoja na uzoefu wake kama mke wa rais  wakati wa Mkutano huo wa Wake wa Maraisi wa Afrika. Kushoto ni Mama Laura Bush akisikiliza.

Mama Obama akikumbatiana na Mama Laura George W. Bush, Jr. mara baada ya kuzungumza na Wake wa Marais.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Twalib Ngoma akiwakaribisha baadhi ya Wake wa Marais waliotembelea kuona shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo.

Baadhi ya Wake wa Marais wakimsikiliza Dkt. Ngoma alipozungumza nao.

Mke wa Rais wa Sierra Leone, Mhe. Mama Sia Nyama Koroma akimpa pole mmoja wa wagonjwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road

Dkt. Ngoma akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wake wa Marais na wagonjwa.
Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Mstaafu George W. Bush, Jr. pamoja na Mama Salma Kikwete na Mama Laura George W. Bush, Jr. wakati wa Chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Mama Salma kwa heshima ya Wake wa Marais.

Baadhi ya Wake wa Marais wa Afrika wakati wa chakula cha jioni

Mama Laura George W. Bush, Jr. akiwa na Mama Cherie Blair, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza.

Rais Mstaafu wa Marekani, Mhe. George W. Bush, Jr. akiteta jambo na Mhe. Rais Kikwete

Mhe. Rais George W. Bush, Jr. akitoa hotuba wakati wa chakula cha jioni

Wake wa Marais wakijadiliana jambo wakati wa  chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshima yao na Mama Salma Kikwete.

Brassband ikitumbuiza wakati wa chakula cha jioni
Afisa Mwandamizi katika Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Hellen Rwegasira akiwa na mmoja wa wajumbe wakati wa mkutano huo wa wake wa marais.


Picha na Reginald Philip na Olga Chitanda

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.