Monday, July 8, 2013

Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo rasmi na Waziri wa Mambo ya Nje wa India

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati) akiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Bibi Preneet Kaur (hayupo pichani) kabla ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission-JPC) kati ya Tanzania na India unaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro kuanzia tarehe 8-9 Julai, 2013. Wengine katika picha ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. John Kijazi (kulia).
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya India, Mhe. Bibi Preneet Kaur akiwa na ujumbe wake wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo rasmi kabla ya kuanza kwa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India.

Mhe. Kaur akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake rasmi na Mhe. Membe (hayupo pichani). Kulia kwa Mhe. Kaur ni Balozi wa India hapa nchini Mhe. Debnath Shaw.

Mhe. Membe na ujumbe wake wakimsikiliza Mhe. Kaur (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo rasmi kuhusu kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na India.Kulia kwa Mhe.Membe ni Balozi Gamaha, Bw. Omar Mjenga, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Asia na Australasia na Bw. Thobias Makoba, Msaidizi wa Waziri.Kushoto kwa Mhe. Membe ni Mhe. Balozi Kijazi na Bw.Clifford Tandari, Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango.
Mazungumzo yakiendelea.

Mhe. Membe na Mhe. Kaur wakielekea kwenye ufunguzi rasmi wa mkutano wa Tume ya Ushirikiano kati nchi hizi mbili.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.