|
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb)
akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Mhe. Monica
Nduva alipomtembelea Ofisini kwake jijini Arusha.
|
|
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb)
akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Mhe. Monica
Nduva alipomtembelea jijini Arusha . |
|
mazungumzo yakiendelea
|
|
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb) katika picha na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Mhe. Monica
Nduva alipomtembelea Ofisini kwake jijini Arusha. |
NAIBU WAZIRI LONDO AMTEMBELEA KATIBU MKUU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb)
ametembelea Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Mhe. Monica
Nduva Ofisini kwake tarehe 13 Agosti 2024 jijini Arusha.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Londo alimuhakikishia Mhe. Nduva
ushirikiano na kumuelezea kuwa Tanzania itashiriki katika masuala yote
yanayohusu Jumuiya ya EAC kwa uzito unaostahili.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kujitambulisha na kufahamiana baada ya
Mhe. Londo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika
mwezi Julai 2024.
Mhe. Londo aliongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.