Friday, August 9, 2024

WAZIRI KOMBO AJITAMBULISHA KWA RAIS WA ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) Ikulu, Zanzibar.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), pamoja na Manaibu wake, Mhe. Cosato Chumi (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dennis Londo (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki; wamefanya ziara ya kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu Zanzibar.

Katika utambulisho huo, viongozi hao wamemuhakikishia Rais Mwinyi kuendelea kushirikiana kwa karibu na kuhakikisha kuwa maslahi ya pande zote mbili—Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yanapewa kipaumbele.

Ziara hii ni hatua muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano kwa manufaa ya wananchi wote wa Tanzania, ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni Wizara ya Muungano.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) Ikulu, Zanziba
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) akijitambulisha kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) Ikulu, Zanziba
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb.), akijitambulisha kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu, Zanzibar
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.