washiriki wakifuatilia ufungaji wa Mkutano wa kwanza wa Elimu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Maadhimisho ya mwaka wa elimu wa AU uliofanyika jijini Arusha tarehe 12-15 Agosti,2024. |

Picha ya pamoja na Meza Kuu wakati wa ufungaji wa Mkutano wa kwanza wa Elimu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Maadhimisho ya mwaka wa elimu wa AU uliofanyika jijini Arusha tarehe 12-15 Agosti,2024. |

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amefunga
rasmi
Mkutano wa kwanza wa Elimu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Maadhimisho
ya mwaka wa elimu wa Umoja Afrika uliofanyika jijini Arusha.
Akizungumza katika hafla hiyo Prof. Mkenda amezitaka nchi wanachama
kuandaa mpango kazi utakaoonesha namna bora ya kutekeleza maazimio
yaliyotokana na mkutano huo ili kuhakikisha yanafanyiwa kazi kwa
ukamilifu.
Pia ametaka kuhakikisha mafanikio yote yaliyopatikana katika maadhimisho
ya mwaka wa elimu wa AU yanasherehekewa na kutafakari jinsi ya kuwa na
mifumo bora zaidi ya utoaji elimu kwa vijana na hivyo baada ya miaka
miwili mkutano ujao uone matunda ya mkutano huo.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Kisekta na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa
Sudan Kusini Mhe. Awut Deng Achuil alıtoa wito wa kuchukua hatua na
kujitoa zaidi ili kuhakikisha malengo na maazimio ya mkutano
yanatekelezwa kwa vitendo na ameipongeza Tanzania kwa kuwa mwenyeji pamoja na
Sekretarieti ya EAC na nchi wanachama kwa kuandaa mkutano huo kwa
mafanikio makubwa.
Mkutano huo wa kwanza na wa aina yake kufanyika katika ukanda wa Afrika
Mashariki ulijumuisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka Serikalini na
sekta binafsi umejadili na kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na fursa
na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki na Bara la Afrika kwa ujumla.
Kufanyika kwa mkutano huo ni utekekezaji wa maamuzi ya Mkutano wa 15 wa
Baraza la Kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki la Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Utamaduni na Michezo; na Umoja wa Afrika.
Mkutano huo wa elimu na Maadhimisho uliwakutanisha Mawaziri wa Elimu
kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wageni mashuhuri
wakiwemo Wawakilishi wa Nchi mbalimbali kama Jamhuri ya Watu wa China;
Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Kikanda na Kimataifa zinazojihusisha na
agenda ya kuendeleza sekta ya elimu kama vile Umoja wa Ulaya (EU),
Umoja wa Afrika (AU), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto
(UNICEF), Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS),
Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Afrika (ADEA), Taasisi ya Haki Elimu, na
Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ).
Mkutano huo pia uliwakutanisha Wadau wa
elimu zaidi ya 600 kutoka Nchi Wanachama, Taasisi za elimu, Mashirika
yasiyo ya kiserikali, Sekta binafsi, Mashirika ya kimataifa, Asasi za
kiraia waliokutana kutathmini, kubadilishana uzoefu wa mbinu bora za
uendelezaji wa sekta ya elimu.
Mkutano huo uliandaliwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
kwa kushirikiana na Nchi wanachama, taasisi zisizo za kiserikali , wadau
wa maendeleo na bhana vya elimu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
ulianza tarehe 12 hadi 15 Agosti 2024.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.