Tuesday, October 13, 2015

Waziri Membe aongoza Siku ya Kilele cha Umoja wa Mataifa.

Mgeni Rasmi wa siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe (Mb.), akitoa hotuba baada ya kupandishwa kwa Bendera ya Umoja wa Mataifa, maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 24-10-2015.
Mgeni Rasmi Mhe Bernard Membe, akisikiliza wimbo wa Taifa kabla ya kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwaajili ya maadhimisho hayo.
Mgeni Rasmi wa siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamilius Membe,akikagua gwaride la heshima kabla ya kupandishwa kwa bendera ya Umoja wa Mataifa.
Askari akipandisha bendera ya Umoja wa Mataifa katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo tarehe 13-10-2015 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika siky 11 kabla ya tarehe halisi kwa sababu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015.
Askari wakiwa wamesimama wima huku wakishuhudia Bendera ya Umoja wa Mataifa ikipandishwa.
Bendera ya Umoja wa Mataifa ikiwa tayari imepandishwa na kupepea pamoja na Bendera ya Tanzania.
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa akiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,tayari kwa kuhudhuria siku ya kilele cha Umoja wa Mataifa.

Rais Mkapa akisalimiana na baadhi ya maofisa wa Umoja wa Mataifa mara tu baada ya kuwasili viwanjani hapo.
Mgeni Rasmi wa siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb), akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,tayari kwa kuongoza kilele cha sherehe za kuzaliwa kwa Umoja wa Mataifa.

Mhe. Bernard Membe akisalimiana na baadhi ya maofisa wa Umoja wa Mataifa mara tu baada ya kuwasili viwanjani hapo.
 Mhe. Membe akisalimiana na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa, mara alipowasili meza kuu.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez, akimkaribisha  Mgeni rasmi, Mhe. Bernard Membe.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akitangaza utaratibu wa sherehe fupi za maadhimisho hayo.


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim, akiomba dua kabla ya shughuli rasmi kuanza. 
Mwakilishi wa madhehebu ya KKKT, akifanya maombi kabla ya kuanza rasmi kwa shughuli za kilele hicho cha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

Mgeni Rasmi wa siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb), akitoa hotuba kwenye maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 24-10-2015.

Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa akitoa hotuba katika siku ya kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa Umoja wa Mataifa.Maadhimisho hayo yamelazimika kufanyika leo tarehe 13-10-2015 ili kupisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 25-10-2015.
 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez,akitoa hotuba yake kwenye maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 24-10-2015.

Wanafunzi wa shule maalumu ya watoto wenye ulemavu wa kusikia, wakicheza wimbo maalumu kama ujumbe wao kwa Umoja wa Mataifa.
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari Jitegemee pamoja na shule nyingine za hapa mjini Dar es salaam nao wakiimba wimbo maalumu wa kuelezea malengo mapya ya maendeleo endelevu yaliyozinduliwa Septemba 2015 mwaka huu Jijini New York Marekani.
 Wanafunzi hao wa shule ya Sekondari Jitegemee, wakitoa heshima kwa Mgeni rasmi pamoja na jukwaa kuu kwaujumla baada ya kumaliza kuwasilisha ujumbe wao kwa Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiendelea kuongoza sherehe hizo
 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez, akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi wa siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamilius Membe, kwa kutambua mchango na ushirikiano wake uliotukuka kwa kipindi chote alichofanya kazi kama Waziri  wa Mambo ya Nje.
 Mhe. Membe akimshukuru Bw. Alvaro kwa zawadi hiyo.
 Waziri Membe alitumia siku ya kilele hicho kuwashukuru Mabalozi wote  kwa ushirikiano wao waliompatia kwa kipindi chote alichofanya nao kazi na kuwaaga rasmi kama Waziri wa Mambo ya Nje.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu pamoja na Viongozi wa dini, mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya siku hiyo ya Kilele cha Umoja wa Mataifa. 

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu pamoja na Wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini, mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya siku hiyo ya Kilele cha Umoja wa Mataifa. 

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu pamoja na Waheshimiwa Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya siku hiyo ya kuzaliwa  Umoja wa Mataifa. 

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu pamoja na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo. 
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu pamoja na Maofisa wa Umoja wa Mataifa, mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa.
 Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu pamoja na Wanafunzi, mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo. 
========================
PICHA NA REUBEN MCHOME. 
========================

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.